Abiria 2 Waislamu wasio na hatia 'wasababisha' kukatizwa kwa safari ya ndege Marekani:

Wanaume wawili Waislamu nchini Marekani wametaka uchunguzi kufanywa baada ya kusema kwamba walibaguliwa kidini katika ndege moja iliokuwa ikielekea mjini Dallas.

Abderraoof Alkhawaldeh na Issam Abdallah wamedai kwamba safari yao ilifutiliwa mbali kwa kuwa abiria hawakufurahia kusafiri na wanaume hao.

''Ilikuwa aibu kubwa katika maisha yangu'' , bwana Abdalla aliambia maripota.

Taarifa ya kampuni hiyo ya ndege ilisema kuwa wasiwasi uliowakabili abiria wa ndege hiyo ulisababisha kufutiliwa mbali kwa safari ya wawili hao.

'Marekani na washirika wake wote wana jukumu la kutilia maanani usalama na wasiwasi wa kiusalama wa wafanyakazi na abiria'' , ilisema katika taarifa.

Ni nini kilichotokea katika ndege?

Bwana Alkhawaldeh na bwana Abdallah walitoa madai hayo katika mkutano na vyombo vya habari ulioandaliwa na baraza la uhusiano wa Waislamu wa Marekani na kutangazwa katika mtandao wa Facebook.

Mnamo tarehe 14 mwezi Septemba, wanaume wote wawili waliorodheshwa miongoni mwa abiria watakaosafiri kutoka Birmingham , Alabama kuelekea Dallas Texas katika ndege ya kampuni ya Marekani inayoendeshwa na kampuni ya ndege ya Mesa Airlines.

Walikuwa wakisafiri lkila mtu kivyake, lakini wakatambuana kupitia kundi moja la Kiislamu na kupungiana mikono wakiwa ndani ya ndege.

Mtangazaji mmoja alisema kwamba ndege hiyo ilicheleweshwa na bwana Abdallah akaelekea msalani.

Alipotoka mfanyakazi mmoja wa ndege alikuwa amesimama nje ya choo hicho kama ambaye alikuwa akijaribu kusikiliza kilichokuwa kikiendelea ndani.

Muda mfupi baadaye wafanyakazi hao waliambia abiria kwamba safari hiyo ilifutiliwa mbali na kwamba walipaswa kutoka katika ndege hiyo.

Bwana Alkhawaldeh alisema alisikia mfanyakazi mmoja akimwambia abiria hatua hiyo ilikuwa ya kiusalama.

Baada ya kutoka wawili hao wanasema kwamba walifuatwa na mtu aliyekuwa amevalia nguo za raia , maafisa waliovalia sare za kazi na baadaye na maafisa wa Ujasusi wa FBI.

Aajenti mmoja alimchukua bwana Abdallah katika chumba kimoja cha faragha na kudai kumuuliza jina lake na kazi anayofanya na kusema kwamba mzigo wake utalazimika kukaguliwa tena.

Alipouliza ni nini kilichokuwa kikiendelea , ajenti huyo alidai kwamba wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ndege waliwaita maafisa wa polisi na kusema kwamba hawakuridhika kusafiri naye.

Sababu iliotolewa na ajenti huyo ni kwamba bwana Abdallah aliingia msalani na kupiga maji mara mbili.

Kulingana na bwana Abdalla ajenti huyo baadaye aliomba msamaha na kumwambia kwamba anaweza kwenda kupanda ndege yake .

''Nilihisi kwamba walikuwa wanabagua kabila langu na dini yangu'' , alisema bwana Abdallah.

Abiria wote baadaye walisafiri katika ndege iliofuata isipokuwa wawili hao.

Je kampuni hiyo ya ndege ilisema nini?

'Tumejizatiti kutoa uzoefu mzuri kwa kila mtu anayesafiri nasi,'' Ilisema taarifa ya kampuni hiyo ya ndege.

Wafanyakazi wetu wanashirikiana na Mesa kuangazia kisa hiki na tumewasiliana na bwana Alkhawaldeh na bwana Abdallah ili kuelewa walivyochukulia utendakazi wetu.

Kampuni hiyo ya ndege imekabiliwa na visa vya ubaguzi katika siku za nyuma.

Mapema mwaka huu kampuni hiyo iliomba msamaha baada ya kudaiwa kumwambia abiria mmoja mwanamke kuficha nguo zake ndani ya blanketi.

Na mwaka 2017, muungano wa watu wa rangi NAACP , kundi la haki za kibinadamu lilionya abiria weusi kwamba kampuni ya ndege ya American Airlines huwabagua bila heshima ama katika mazingira yasio mazuri.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?