Adele awasilisha maombi ya talaka dhidi ya mumewe

Adele na Simon Konecki walioana katika ndoa ya siri mwaka 2016

Mwimbaji wa muziki Adele amewasilisha kesi ya talaka dhidi ya mme wake Simon Konecki, kwa mujibu wa nyaraka za kesi zilizowasilishwa katika mahakama nchini Marekani

Mwakilishi wao amesema kuwa wawili hao " wako tayari kushirikiana kwa pamoja kumkuza mtoto wao mpendwa wa kiume ".

Adele alijifungua mtoto huyo wa kiume , Angelo, mnamo mwaka 2012. Aliolewa na Konecki - ambaye ni mwekezaji katika sekta ya benki ambaye aligeuka na kuwa mkuu wa shirika la misaada mwaka 2016 baada ya miaka mitano ya uchumba.

Adele ambaye ni mzaliwa wa kaskazini mwa London ndiye mwanamuziki anayefahamika kwa kuwa juu kwenye chati kwa kwa albamu zake 19, 21 na 25.

Taarifa kuhusu maombi yake ya talaka iliongeza kuwa wawili hao ambao walitangaza kuachana mwezi Aprili waliomba kesi yao iwe ya siri na kwamba hawatatoa maelezo yoyote.

Karatasi za talaka ziliwasilishwa katika mahakama mjini Los Angeles.

Walioana katika sherehe ya siri mnamo mwaka 2016, ambapo Adele aliutangazia umma harusi kwa mara ya kwanza katika hotuba ya kupokea tuzo ya Grammys, mwaka 2017 ambapo alimshukuru mumewe.

Miongoni mwa kazi zake za muziki maarufu alizozitoa ni albamu iliyotolewa mwaka 2008 iliyokuwa na nyimbo kama vile including Chasing Pavements na Hometown Glory, ambayo ilishika namba moja nchini Uingereza.

Alipata tuzo mbali mbali na albamu yake iliyofuatia , 21, ilikuwa ya kwanza kwenye chati za muziki katika nchi 30 zikiwemo Marekani na Uingereza .

Albamu yake ya tatu , 25, ilivunja rekodi ya mauzo kwa kuuza nakala 800,000 na ikaw albamu iliyouzwa zaidi ya mwaka 2015.

Ripoti za hivi karibuni zinasema kuwa Adeleanarekodi muziki mpya , na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 31- alipigwa picha akielekea katika studio kurekodi muziki katika studio mjini New York City mwezi Machi

Konecki, mwenye umri wa miaka 45, aliacha kazi yake katika kampuni ya Lehman Brothers mwaka 2005, na kuanzisha kampuni yake ya maji safi -Life Water. Kampuni hiyo na washirika wake wa msaada The Drop 4 Drop hutoa msaada wa udhamini wa maji safi katika maeneo mbali mbali duniani.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?