Tanzania, DRC, Nigeria na Zambia zaichukulia hatua Afrika Kusini huku taifa hilo likifunga ubalozi wake Nigeria:

Serikali ya Tanzania imesitisha kwa muda huduma ya usafiri wa ndege zake nchini Afrika Kusini hadi hali ya usalama nchini humo itakapotengamaa.

Shirika la ndege ya Air Tanzania lilitakiwa kuwa safari zake zitarejea siku ya Ijumaa tarehe 6 kuelekea Afrika Kusini mara baada ya ndege yake iliyozuiliwa Agosti 23, 2019 kuachiwa kwa amri ya mahakama na kurudi Tanzania.

Lakini kutokana na hali ya usalama nchini humo kutokuwa nzuri, safari hizo zimesitishwa kwa muda.

"Tutasitisha kwa muda usafiri wa ndege hadi serikali itakapofanya mawasiliano na nchi hiyo kwa maandishi kuhakikisha usalama wa abiria na chombo chetu.

Hatuwezi kuwapeleka abiria kwenye nchi yenye fujo. Tutawapa taarifa hali itakapotulia," amesema Kamwelwe katika gazeti la Mwananchi.

Hatua hiyo inajiri baada ya Afrika Kusini kufunga ubalozi wake nchini Nigeria , huku nalo taifa hilo likifunga vituo vyake vya biashara vilivyopo Afrika Kusini

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Afrika Kusini alitaja ghasia hizo kuwa aibu kwa taifa lake.

"Serikali yetu inajutia ghasia dhidi ya maduka yote yanayomilikiwa na wageni ama Waafrika katika mataifa mengine wanaoishi nchini Afrika kusini, kilisema chombo cha habari cha SABC kikimnukuu waziri Naledi Pandor.

Alikuwa ameagiza kufungwa kwa ubalozi wa taifa lake katika mji mkuu wa Abuja na Lagos kufuatia vitisho vilivyowalenga wafanyikazi wake wa kidiplomasia , bi Pandor aliambia Reuters.

Nchini Zambia , kituo maarufu cha redio kimesema kuwa hakitapiga tena muziki wa Afrika kusini kupinga mapigano ya ubaguzi ambayo yanaendelea Afrika Kusini .

"Hot FM imesitisha kupiga muziki aina yoyote ulioimbwa na msanii wa Afrika Kusini," Kituo hicho kimeandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Facebook.

"Mataifa yote ya Afrika yalisimama mstari wa mbele kuisaidia Afrika Kusini walipokuwa na shida," redio hiyo ilisema ikinukuu Umoja wa Afrika.

Wakati wa mapigano dhidi ya ubaguzi wa rangi , makao ya chama tawala cha Afrika Kusini(ANC) yalikuwa Zambia .

"Afrika ni moja ingawa sasa wenzetu Afrika Kusini ndio wameamua kuleta ubaguzi tena,

Tunapinga uvamizi wa chuki za kibaguzi dhidi ya ndugu zetu unaoendelea katika katika nchi hiyo ."

Siku ya Jumatano , maduka kadhaa katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka yalifungwa wakati wanafunzi walipoingia barabarani kuandamana kupinga vurugu zinazoendelea Afrika Kusini,

Chama cha mpira wa miguu kilisitisha mechi ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini ambayo ilitarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi mjini Lusaka.

Mara baada ya vurugu hizo kutokea Afrika Kusini imefunga ubalozi wake katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja na kufunga vituo vyake vya biashara vilivyopo Afrika kusini

Raia wa Nigeria ndio walihusishwa zaidi katika ghasia za ubaguzi wa wageni mara baada ya ghasia za ubaguzi zilipoanza mjini Johanesburg.

"Baada ya kupata taarifa za vitisho kutoka kwa wanaijeria , hivyo tuiamuka kufunga kwa muda mpaka hali itakaporejea kuwa shwari," AFP ikimnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lunga Ngqengelele

Mpango wa kidiplomasia ulimalizika siku ya jumatano, waziri alisema.

Takriban watu 423 wamekamatwa kufuatia ghasia za uporaji kote mjini Johannesburg a na jimbo hilo , kwa mujibu wa maafisa.

Raia wa Nigeria wanaoishi Afrika Kusini wamepewa ofa ya ndege za bure kurejea nyumbani kukwepa vurugu za kibaguzi zinazoendelea Afrika Kusini.

Wizara ya mambo ya Nje ya Nigeri imesema mmliliki wa Shirika la Ndege la Air Peace yupo tayari kuwasafirisha bure wale wote watakaotaka siku ya Ijumaa.
"Wote watakaotaka huduma hiyo wanashauriwa kuwasiliana na Ubalozi wa Nigeria jijini Pretoria na ofisi ndogo za ubalozi jijini Johannesburg jwa matayarisho muhimu," taarifa ya wizara imeeleza.

Huko Jamuhuri ya Kidemokrasi ya kongo pia maandamano yanafanyika mjini Kinshasa kupinga ghasia za uporaji dhidi ya raia wa kigeni.


Raia hao wa DRC wanasema kwamba kile kinachoendelea Afrika Kusini sio kitu kizuri kabisa ndio maana wamea mua kwenda kwenye ubalozi wa nchi hiyo kuonyesha hisia zao.

"Si kweli kwamba ndugu zetu wanaoishi Afrika Kusini wanaoiba kazi zao, hiyo sio kweli kabisa. Tunawaomba waache wanachokifanya sisi wote ni ndugu.

Sheria yao inaruhusu watu wafanye kazi kwao, hawapasi kutufanyia sisi hivyo sisi ni ndugu na tuliwasaidia sana Afrika Kusni wakati wanapambana na ubaguzi wa rangi, nchi zote za Afrika zilisaidia, kwa nini sasa iwe hivi..." alisema raia mmoja wa DRC.

Mwaka 2007 baadhi ya raia wa Kisomali walijihami dhidi ya uvamizi wowote wa Wageni mjini Pretoria katika eneo la Marastabad nchini Afrika Kusini.

Kundi hilo lilikuwa linakabiliana na kundi jingine la raia wa Afrika kusini lililoongoza ghasia dhidi ya wahamiaji.

Hatahivyo maafisa wa polisi waliingilia kati na kuwatimua kwa kutumia ndege aina ya helikopta pamoja na risasi za mipira.

Takriban watu wawili walijeruhiwa na risasi hizo za mipira wakati polisi walipokuwa wakitawanya maandamano dhidi ya wageni nchini humo.

Mpiga picha mmoja alipigwa risasi mbili za mipira mgongoni alipokuwa akirudi nyumbani kutoka shule.

Licha ya Bwana Mashaba kusema kuwa ghasia hizo hazina nafasi katika taifa hil,o wanaharakati wa shirika hilo wanadai kuwa matamshi yake kwamba wahamiaji nchini humo ndio wanaohusishwa na uhalifu ndio yaliosababisha ghasia hizo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?