Fatma Karume aapa kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kumvua uwakili:

Wakili wa Tanzania fatma karukme aliyevuliwa uwakili siku ya Ijumaa ameapa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo alioutaja kua kinyume na sheria.

Akizungumza kwa njia ya simu na Newsday Swahili Bi karume alisema kwamba Jaji wa mahakama aliyetoa uamuzi huo hakufuata taratibu yoyote kabla ya uamuzi huo huo.

Alisema kwamba pia atakwenda katika kamati ya mawakili ili kutoa malalamishi yake kuhusu uamuzi huo ambao anasema kwamba unakiuka haki zake za kisheria.

Hakunipa haki yangu ya kusikilizwa , hakunipa notisi yoyote ili kusikiliza malalamishi kuhusu wakili wangu , amevuruga kabisa sheria, alisema bi karume ambaye ni ,mtetezi wa haki za kibinaadamu mbali na kuwa wakili wa kikatiba.

''Eti pia kaamua kwamba Ado Shaibu amlipe fidia rais Magufuli inawezekanaje hiyo ilihali rais anatetewa na wakili mkuu ambaye analipwa na kodi ya mwananchi''.

Hatahhivyo wakilki huyo amesema kwamba hashangazwi na uamuzi uliotolewa kwa kua hata aliyekuwa mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu hakupatia haki yake alipowasili mahakamani kuomba haki yake.

''Katika sheria unapotoa kauli ambazo ambazo zimezua malalamishi uande wa serikali ni lazima upewe notisi uende kujitetea, useme ni kwa nini umesema mambo hayo nayo serikali isema ni kwa nini kauli hizo hazihitajiki , lakini mimi sijapewa haki hizo fesheli kaamua alivyootaka''.

Na punde tu baaada ya uamuzi huo wafuasi wa wakili huyo walijitokeza mitandaoni na kumuunga mkono wakisema wako naye bega kwa bega

Siku ya Ijumaa wakili huyo alisimamishwa kufanya kazi za uwakili katika eneo la Tanzania bara.

Maamuzi hayo yametolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na mwanaJF Ado Shaibu akipinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG).

Mahakama Kuu imeamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili kwa madai ya kushambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Sababu yake ilitajwa kuwa kile alichokizungumza katika kesi iliofunguliwa na katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano katika chama cha Wazalendo, Ado Shaibu kupinga uteuzi wa Mwanasheria mkuu wa serikali Dkt Adelarus Kilangi aliyeteuliwa na rais John Pombe Magufuli mnamo February Mosi 2018.

Shaibu alisema kwamba mawakili wa serikali walilalamikia maneno yalioandikwa na Fatma wakati walipokua wakifungua kesi hiyo mahakama kuu.

Alinukuliwa akisema: Hata iwapo kesi hii itashindwa ataendelea kupambana nayo, rais akiondoka madarakani mwaka 2020 au kama ataondoka 2025 au kama mahakama itabadilika ataendelea kupambana''.

Mimi sishangai kuvuliwa au kusimamishwa uwakili ,pengine Mungu hataki niendelee kuwa huko , pemngine anataka niingie kwenye siasa au nifanye kingine tofauti. Nitakaa na kutfakari alinukuliwa na mwananchi akisema.

Hatahivyo amesema kwamba hatua hiyo haitabadili maisha yake bali itabadilisha uwezo wake wa kusimamia kesi za kikatiba , akibainisha kuwa bado ni wakili Zanzibar, ana ofisi na ataendelea kusimamia kesi za kikatiba.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?