Tetesi za soka jumanne barani Ulaya:

Klabu ya Celtic ya Uskochi inaweza kujaribu kumsajili kiungo wa klabu ya Tottenham na Kenya Victor Wanyama, 28, mwezi Januari, kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo Neil Lennon. Wanyama aliwika na Celtic kabla ya kutimkia England, na sasa kocha wa Tottenham ameshaeleza kuwa hana haja naye.

Winga wa Chelsea na Brazil Willian anataka kusalia kwenye uga wa Stamford Bridge, lakini klabu hiyo hata hivyo bado haijampatia nyota huyo mwenye miaka 32 mkataba mpya. 

Beki wa Ajax na Uholanzi Joel Veltman, 27, amebainisha kuwa alitaka kujiunga na klabu ya West Ham United ya England katika dirisha la usajili lililopita lakini mabingwa hao wa Uholanzi hawakumruhusu kuindoka.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?