Ujumbe mfupi kutoka kwa Lionel Messi huenda ulivuruga mpango wa Barcelona kumsajili tena mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, kutoka klabu ya Paris St-Germain.
Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi angelifanikiwa kumpata Neymar msimu huu ikiwa dau la kuvunja rekodi la euro milioni 300 sawa (£272m) lingemfikia.
CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo kuhusu taarifa Author, Watu wengi huko Somaliland wanaamini kwamba Marekani, chini ya rais ajaye Donald Trump, itakuwa nchi ya kwanza duniani kuitambua jamhuri hiyo iliyojitangazia uhuru wake. Eneo hilo lilijitangazia uhuru miaka 33 iliyopita baada ya Somalia kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. "Donald ni mwokozi wetu. Ni mtu mwenye hekima. Mungu ibariki Marekani," anasema mwanafunzi wa chuo kikuu Aisha Ismail. Anazungumza nami kutoka Hargeisa, mji mkuu wa Somaliland - jiji lililo umbali wa kilomita 850 (maili 530) kaskazini mwa Mogadishu, Somalia. Kwa wale walio Mogadishu, Somaliland ni sehemu ya Somalia. "Nina shaka kwamba Donald Trump anaijua Somaliland ni nini, au iko wapi," anasema Abdi Mohamud, mchambuzi huko Mogadishu. Pia unaweza kusoma Wakuu wa jeshi la Ethiopia-Somaliland wakutana huku kukiwa na mvutano wa kikanda 9 Januari 2024 Makubaliano ya Ethiopia na Somaliland yatikisa diplomasia katika Pembe ya Afrika 9 Janu...
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Hivi karibuni nchi za Ulaya, Marekani na Canada zimekuwa zikitangaza hatua ya kukata misaada dhidi ya Rwanda, kufuatia kile kinachoelezwa na nchi hizo za Magharibi kwamba inaunga mkono kundi la M23 liloteka maeneo ya mashariki mwa DRC, ikiwemo miji ya Goma na Bukavu. Nchi hizo zinaituhumu Rwanda kuchochea ghasia katika eneo la Mashariki mwa DRC kwa kuwaunga mkono waasi wa kitutsi wa Congo wa kundi la M23, tuhuma zinazokanushwa vikali na Rwanda. Lakini je, Rwanda inaweza kujitegemea bila misaada? Kujibu swali hili ni vyema kuelewa ni kwa namna gani Rwanda inategemea misaada kutoka mataifa ya kigeni kwa ajili ya kuendesha uchumi wake. Kulingana na takwimu za Benki ya Dunia, Rwanda ilikadiriwa kutegemea kwa kiasi kikubwa misaada ya kigeni mnamo 2024, huku makadirio yakionyesha kuwa misaada na mikopo kutoka nje inaweza kuchangia na karibu 27% ya jumla ya bajeti ya taifa hilo. Inakadiriwa kuwa Rwanda inapokea zaidi ya dola bilioni 1 ya msaada wa kigeni Pia una...
Ubalozi wa Marekani umesema kwamba haumuungi mkono mgombea yeyote au chama chochote katika uchaguzi ujao wa Tanzania. ''Tunaunga mkono mchakato wa kweli wa uchaguzi huru, wa haki na wenye uwazi, kabla, wakati na baada ya siku ya uchaguzi. Hii ni pamoja na usalama wa wagombea wote, kuheshimiwa kwa utawala wa kisheria na hali ya mamlaka na vyombo vilivyopewa wajibu wa kusimamia na kuendesha uchaguzi kutokupendelea kabisa upande wowote'', ulisema ubalozi huo. Kupitia taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya ubalozi wa taifa hilo nchini Tanzania, ubalozi huo hatahivyo umesema kwamba utafuatilia kwa karibu matendo ya watu wanaoingilia na kuvuruga mchakato wa kidemokrasia au kuchochea vurugu dhidi ya raia. Aidha ubalozi huo umesema kwamba unaunga mkono wito uliotolewa na wagombea wakuu wa kuwepo kwa mchakato wa uchaguzi wa amani na wenye uwazi. ''Tunatoa wito kwao na kwa wafuasi wao kuchukua hatua kutanzua hali ya usalama inayojengeka na kuepuka ma...
Maoni
Chapisha Maoni