Kipindi cha radio kilichowarudisha nyumbani watoto walionusurika mauaji ya kimbari Rwanda:

Kutokana na wazo hilo iliamuliwa hatua ya kuanzisha kipindi cha dakika ambacho kitakua kikipeperushwa hewani na Newsday Swahili kikiwalenga wasikilizaji wa Rwanda na mataifa yalio karibu.

Kipindi hicho kilianza kwa Taarifa ya Habari na kufuatiwa na sauti za watu wanaowatafuta jamaa zao.

Ukweli ni kwamba haikua rahisi kutayarisha kipindi hicho lakini kwa ushirikiano na mashirika yasiokua ya kiserikali kama vile Shirika la Msalaba Mwekundu, Save the Children na Umoja wa Mataifa sauti zilizorekodiwa kutoka kwa wahasiriwa ziliwasilishwa katika studio za Newsday Swahili

"Tulipeperusha hewani sauti za watu kutoka kambi hizo za wakimbizi ," anaeleza Mugenzi, ambaye pia alikua mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho kilichokua kikiendeshwa na watangazaji wawili.

Hatimaye tulipewa jina la Gahuzamiryango, likimaanisha "muunganishi wa familia" na mara ya kwanza ilitangazwa kwa mara ya kwanza miaka 25 iliyopita.

Kipindi hicho kilitarajiwa kumalizika baada ya miezi mitatu. Lakini muda huo ulifikia kikumo na kuendelea mbele.

Mara ya mwisho Rene alikutana na familia yake walikua wanarejea nyumbani Rwanda. Na wakati huo walikua wametoweka.

"Unaweza kutafakari hali ya mtoto aliyepotea?" aliuliza. "Nilikua nalia tu, nilipoteza matumaini. Niliona watu wengi lakini sikuona mtu yeyote wa familia yangu."

Kufikia wakati alipatikana na wafanyikazi wa kutoa misaada alikua amepoteza uwezo wa kuzungumza.

"Waliniuliza jina langu na mahali nilikotoka lakini kutokana na uoga na mfadhaiko nadhani nilishindwa kujieleza."

Hakuweza kuzungumza tena kwa miezi kadhaa, alihamishiwa makaazi ya watoto mayatima waliokabiliwa na hali kama yake, na ambao wamejipata peke yao duniani.

Lakini - baada ya kupata utulivu kutokana na familia yake mpya iliyomchukua na kumlea- sauti yake iliwafikia wengi kupitia matangzo ya redio.

"Majirani zangu walinifikia baada ya kusikia jina langu redioni," anakumbuka. Alienda nyumbani kwa majirani zao kujisikilizia mwenyewe matangazo hayo.


"Sikuweza kukumbuka jina langu, lakini nilikumbuka jina na ndungu yangu mdogo," Mugabo alifichua hayo, huku akionesha Newsday Swahili picha ya wavulana wawili ambao Red Cross iligundua wanaishi peke yao nchini DR Congo.

Lakini hiyo haikutosha: nyumbani Kigali, mjomba wao Theogene pia alisikia matangazo ya redio.

"Niliposikia matangazo hayo redioni nilihisi kama nimepata ujumbe kutoka mbinguni ," alisema, kumbukumbu hiyo inamfanya atabasamu karibu robo ya krane baadae.

Hatua ya kusikia majina ilikuwa sehemu ya kuwarejesha nyumbani watoto hao. Nchi ilikuwa bado inakabiliwa na ghasia na barabara zilikuwa hatari.

Lakini hofu kubwa ya vijana hao ilikua uoga wa kurudi nyumbano.

"Niliona barua ya mjomba wangu aliyekuwa Rwanda na aliyetaka kutuona. Lakini nilikataa," Mugabo anasema.

"Nilishuhudia baba yangu akifariki, Nilimuona mama yangu akifariki, kwa nini nirudi huko?"

Halafu suala lingine: nikuwa mjomba wake alikua askari wa Rwandan Patriotic Front - wanajeshi waasi wa wa Kitutsi waliochukua uongozi wa Rwanda, na kumaliza mauaji ya kimbari.

Mugabo alikuwa akifundishwa kwamba wanajeshi hao, ni mende waliokua na mkia.

Lakini mjomba wake alikua na nafasi moja ya kujieleza: alituma picha yake akiwa na ndugu yao mwingine. Picha hiyo iliwashawishi: baada ya kuishi msituni kwa mwaka mmoja, Mugabo na Tuyishimire hatimae walikubali kwenda nyumbani.


Rene haelewi kwa nini hakufanya lolote aliposikia jina lake redioni miakayote iliopita. Pengine, ni uoga: alifahamu fika maisha yake yalikua mazuri na familia yake mpya. Ambayo ahuenda ilikua mahali salama.

Hata hivyo, alikua na matumaini huenda kuna mtu wa familia yake aliyekua anamtafuta.

"Wazo hilo lilikuwa akilini mwangu," alisema. "Nitaka tena kusikia jina langu redioni lakini hilo halikufanyika."

Hatua iliyomfanya kusalia na jina lake licha ya mama yake mlezi kupendekeza abadilishe jina kwa sababu ni mmoja wa familia hio.

Na baada ya kujiunga na mtandao wa kijamii wa Faceboo zaidi ya miaka 15 iliyopita anatafakari ikia kuna mtu atamtambua, na haikuchukua muda mrefu alipata jibu.

"Niliweka jina langu mtandaoni siku ya Jumamosi na ilipofika Jumapili,walinipata ."


"Mwaka 1995 tulijaribu kumtafuta," mjomba wa Rene, Charles aliiambia BBC. "Hatukumpata, lakini hatukumsahau. Tulidhani amefariki. Tulimweka katika kumbukumbu ya kihistoria.

"Na miaka 18 baadae, ni kama miujiza kwetu kubaini kuwa yungali hai."

Ni ndugu yake Rene, Olivier ambaye alimpata kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook - Ni yeye aliyeifahamisha familia yake kuwa kijana wao aliyetowekaamepatikana.

"Unafanana na ndugu yake mdogor," Olivier alimwambia Rene mara ya kwanza walipokutana. "Ni wewe sina shaka na hilo."

Hii ilikua mara kwanza tangu wawili hao walipotenganishwa miaka yote hiyo amabyo Rene aligundua ndugu yake aliponea Matangazo ya Redio sio njia pekee iliyotumiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu na mashirika mengine ya kutoa misaada ya kibinadamu kuwaunganisha watoto waliopotea na familia zao.

Picha na majina ya watoto zilisambazwa kutoka kijiji kimoja hadi kingine ili kutafuta jamaa zao.

Mwisho wa mpango huo, Espèrance Hitimana, ambaye sasa ni msimamizi wa kulinda data katika Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu mjini Kigali, anakadiria walifanikiwa kuwaunganisha watu 70,000 .

Lakini dhughuli hiyo bado inaendelea.

"Bado tunapoke visa kama mbili au tatu kwa mwezi,"anasema. "Visa vingine tunafanikiwa kupata familia. Katika visa ambavyo hatuna taarifa yoyote hatuna budi kuwaeleza hatuna la ziada."

Katika Idhaa ya Newsday Swahili
ya Maziwa makuu, japo makala ya kuunganisha familia zilizotengana - yalisitishwa.

Siku hizi inajivunia kipindi cha mjadala ambayo imeelekeza darubini yake katika mawasiliano ua kidigitali.

Mugenzi - ambaye anaongoza Idhaa ya BBC Great Lakes Service iliyobuniwa baadae - anaelezea kwa furaha isiyokua na kifani kile walichofikia katika kipindi cha miaka 25 iliopita.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?