Mambo matano ya kujifunza katika Safari ya Papa barani Afrika:

Papa Francis ameongoza mamia ya watu ya mataifa matatu alipotembelea Afrika ikiwa ni ishara ya kukua kwa kanisa Katoliki barani humo.

Hii ilikuwa ni ziara yake ya nne tangu alikuwa papa mwaka 2013.

Mtangulizi wake Papa Benedict wa XVI alizuru mara mbili Afrika katika kipindi cha uongozi wake wa kanisa hilo.

Mhariri wa dini wa Newsday Swahili aliambatana na Papa Francis katika ziara yake nchini Msumbiji, Madagaska na Mauritius.

1) Upendo kwa maskini

Hii ilikuwa fursa ya Papa kubadilisha mawazo na kupumzika.

Kwani mwaka huu umekuwa wa matukio mengi ambayo yalihatarisha mienendo ya viongozi wa kanisa hilo tangu mwezi Februari.

Hii ilifuatia shutuma za uzalilishaji wa kingono ambazo zimemkabili kadinali George Pell ambaye pia alikutwa na hatia.

Pell ameshitakiwa kifungo cha miaka sita jela kutokana na kukutwa na hatia.

Safari yake Papa barani Afrika , lengo ni kusaidia wahitaji.

Shirika la chakula la umoja wa mataifa linasema 80% ya raia wanaoishi nchini Msumbiji hawawezi kukidhi mahitaji yao ya chakula.

Na 90% ya watu wanaoshi Madagaska hutumia chini ya dola mbili za kimarekani kwa siku.

Nchini Mauritius , wahitaji ni wengi zaidi hivyo Papa alitumia muda huo kusaidia wasiojiweza.

'vijana hasa ndio wanaoteseka na umasikini,' alisema Papa.

Wanakumbana na ukosefu wa ajira, ambayo inahatarisha maisha ya watu siku za usoni.

2) Kutunza mazingira

Papa pia aligusia suala la uhifadhi wa mazingira, mnamo mwaka 2015, aliandaa makala iliyogusia utunzwaji wa mazingira.

Kitabu hiko kiliandikwa 'Laudato Si , Katika nyumba yetu, kitabu ambaco kinawafundisha watu kujali utu na sayari tunayoishi..

Haikuwa bahati tu kuzuru nchi hizi bali kisiwa cha nne kwa ukubwa duniani kimekumbana na changamoto ya mazingira kutokana na kukatwa miti, huku 40% ya misitu ikitabiriwa kupotea miaka 60 ijayo.

Hatari kubwa iliopo hivi sasa katika kisiwa hicho ni kupotea kwa viumbe hai walio adimu duniani lakini wanapatikana katika kisiwa hicho.

Benki ya Dunia inasema Msumbiji imepoteza hekali million 8 ikiwa ni takribani ukubwa wa nchi ya Ureno

Nchini Msumbiji, Papa alilaani tabia ya uporaji inayotokana na uchoyo na tamaa ambayo kwa ujumla haukuwa utamaduni wao hivyo wanapaswa wawe wema kwa watu wote.

Papa aliwaambia watu wa Madagaska kuwa visiwa vya nchi yao vina utajiri wa mimea na wanyama lakini vyote vipo hatarini kutokana na ukataji wa misitu unaoendelea.

Mitu mingi imeharibiwa kutokana na uvuvi haramu na ukataji mbovu wa misitu.

3) Anashikilia ngome ya Afrika katika imani

Waandaaji wa misa hiyo wamesema zaidi ya watu millioni moja waliudhuria misa hiyo, hii ishara kubwa kuwa kanisa la kikatoliki linazidi kukua.

Watu walimshangilia sana kiongozi huyo wa dini mwenye umri wa miaka 82 alipopanda katika altare.

Takwimu za kanisa la katoliki linaonesha waumini wa kanisa hilo wameongezeka million 6.3 kati ya mwaka 2016 na 2018.

Idadi hii inaongeza ile ya waumini million 150 kutoka Afrika.

Idadi ya waumini katika bara la Ulaya na Mashariki ya Ulaya, huku kanisa la Afrika, Kusini mwa Asia na Latini Ya Marekani ikizidi kushuka.

4)kuwakarimu wakimbizi

Safari yake ya mwisho ilichukua masaa mawili kwa ndege mpaka Mauritius.

Na alipofika nchini humo, Papa alihutubia viongozi wa kisiasa na wanadiplomasia ikulu huku akikemea ubaguzi wa rangi na wa dini.

Papa Francis amewataka watu wa Mauritius kuishi kwa umoja na amani.

Aliwasisitiza kuwa wakarimu kwa wakimbizi kwa kuwapa fursa za ajira na namna za kujipatia kipato, kuwasaidia kama vile mababu zao walivyokuwa wakarimu miaka ya nyuma.

Lengo kuu la papa kudhuru nchini Mauritius ni kuhimiza raia wa Mauritius kuwapa fursa za ajira wakimbizi hao kwani kufanya hivyo pia itainua uchumi wa nchi humo



 5) Na, alionesha ukarimu wake

Kila wakati kiongozi huyo mkubwa wa dini anaposafiri na waandishi wa habari, huenda sehemu ya abiria na kujumuika na kubadilishana nao mawazo.

huwaeleza kwa ufupi juu ya nchi ambayo wanaenda kuzulu, hii huchukua si Zaidi ya robo saa. Na baadae kupita na kuzungumza na abiria ambao anakuwa ameambatana nao.

.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?