Papa Francis awataka viongozi kutoa fursa kwa wote:


 Francis amewaambia raia wa Msumbiji kuwa wanahitaji kukuza amani yao na kuhakikisha kuwa inadumu

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani alikuwa akizungumza katika ziara yake ya siku moja nchini Msumbiji , abako hivi karibuni mkataba wa amani ulimaliza rasmi miaka ya vita vya wenyewe kwa wenyewe

Amani lazima iwe ada na maridhiano yawe ndio njia bora ya kukabili magumu ya nchi ,"amesema Papa.

Amesema amani ni kama "ua laini " na huhangaika kuchanua katika "ardhi yenye mawe ya ghasia ".

Ili amani iwepo ya kudumu Papa amesema viongozi wa nchi sharti wazuwie aina yoyote yaushabiki na kupigania kutoa hfursa sawa kwa wote - kufanya kinyme cha hayo kunaweza kuhatarisha amani.

"Bila fursa sawa, aina tofauti za uchokozi na mizozo vitapata ardhi ya rutba ya kukua na hatimae kulipuka, " amesema.

Baadae alipokutana Papa Francis alipokutana na viongozi wa vijana kutoka dini mbalimbali katika mji mkuu , Maputo, aliwaambia: "wengi miongoni mwenu mlizaliwa wakati wa amani, amani iliyopatikana kwa njia ngumu, kwamba haikuwa kila mara rahisi kufikiwa na ilichukua muda kuipata.

"Amani ni mchakato ambao wewe pia unatolewa wito kuiendeleza, kwa kuwa tayari wakati wowote kuwafikia wale wanaokabiliwa na hali ngumu.

Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, ameanza ziara rasmi ya kihotoria Barani Afrika wiki hii - akiwa anazitembelea Msumbiji, Madagascar na Mauritius.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?