Erick Kabendera: Mwandishi anayeshikiliwa Tanzania afanyiwa vipimo:

Mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Erick Kabendera, anayetuhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, ameieleza mahakama nchini humo kuwa ameanza kupelekwa hospitali.

Kabendera alionekana akiuvuta mguu wake, na kuwa kwenye maumivu wakati alipopandishwa kizimbani Septemba 12, na mawakili wake kuiambia mahakama kuwa mteja wao ana matatizo ya kupooza mguu wa kulia na pia kupumua kwa shida.

Hii leo kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Kabendera amethibitisha kuwa jana Jumanne Septemba 17, 2019 alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Amana na amefanyiwa kipimo cha X Ray kwenye mgongo pamoja na kipimo cha damu.

Nashukuru jana nilifanikiwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Amana na nilifanyiwa kipimo cha X Ray kwenye mgongo wangu na majibu yametoka," amedai Kabendera.

Kabendera amedai alikuchukuliwa kipimo cha damu na majibu yake bado hajapewa, na yanasubiriwa ilia aanze matibabu.

Pia ameieleza mahakama kuwa bado ana maumivu makali katika mguu wake.

Upande wa mashataka umedai kuwa bado haujakamilisha upelelezi na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Kisutu Agustine Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 1, 2019.

Mashtaka dhidi ya Kabendera

Kabendera alipandishwa kizimbani Agosti 5 na kusomewa mashtaka matatu ya ubadhirifu wa kiuchumi .

Katika mashtaka hayo Kabendera anatuhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini Tanzania, shtaka la pili ni la kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja sabini za kitanzania.

Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.

Kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa, Kabendera anadaiwa kuyatekeleza hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakamani.

Makosa yote hayana dhamana na Kabendera anaendelea kusota rumande.

Kumekuwa na ukosoaji ndani na nje ya Tanzania juu ya kesi hiyo, huku wanaharakati wakiitaka serikali ya Tanzania kufuta mashtaka dhidi ya mwanahabari huyo.

Awali alikamatwa na polisi pamoja na Idara ya Uhamiaji nchi hiyo wakathibitisha kuwa wanamchunguza juu ya utata wa uraia wake.

Ofizi za ubalozi wa Marekani na Uingereza nchini Tanzania wametoa tamko la pamoja Agosti 9 na kulisisitizia mtandaoni tena baada ya wiki mbili wakitaka haki za Kabendera kulindwa.

"Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni -- jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai," ubalozi wa Marekani na Uingereza walieleza kwenye tamko lao la awali.

Wiki mbili baadae wakasisitizia kuwa:"Tunaendelea kufuatilia kesi ya Erick Kabendera. Haki za kisheria ni haki ya raia wot, na kuhakikisha upatikatnaji wa haki hiyo ni wajibu wa serikali zote."



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?