Ulama: Mchezo wa jadi unaorudi kwa kishindo baada ya kupigwa marufuku karne tano zilizopita;

Kundi la vijana wa Mexico linafufua mchezo wa jadi wa mpira uliowahi kuchezwa na jamii za Aztecs, Maya and Incas.

Mchezo wa 'Ulama' ulichezwa huko Mesoamerica zaidi ya karne tano zilizopita kabla ya watawala wa Uhispani kuwasili katika eneo hilo mnamo 1519.

Wachezaji wanaovaa mikanda maalum na vitambara vy kujifinika sehemu zao za siri wanasukuma mpira kwa viuno vyao. Mpira wenyewe unaweza kuwa na uzito wa hadi 4kg.

Wakati inaaminika kuwa kuna aina tofauti za mchezo huo, mara nyingi ilidhaniwa ulihusisha timu hasimu zilizokabiliana ana kwa ana, kila upande ukiwa unasalia katika sehemu nusu ya upande wake na kupasisha mpira kutoka timu moja hadi nyingine pasi kuuangusha mpira.

Katikaaina nyingine za mchezo huo, ulichezwa katika eneo lililozungukwa kwa kuta za mawe lenye mduara uliomfano wa vikapu kama katika mpira wa vikapu.

Wakati mchezo wa Ulama unafufuliwa katika baadhi ya maeneo ya kale Mexico, mji mkuu hauku na sehemu ya kuchezea mchezo huo hadi hivi karibuni wakati kumejengwa eneo la kitamaduni katika sehemu ya kutupa taka katika mtaa wa Azcapotzalco.

Emmanuel Kakalotl ni mkufunzi katika uwanja huo mpya. "Mchezo huu ulikuwa umesahaulika," ameliambia shirika la habari la AFP.

"Ulipinduliwa miaka 500 iliyopita, lakini sasa tunaufufua upya," anafafanua.

Wanawakepia wanaingia katika utamaduni huu wa jadi.

Beatriz Campos mwenye umri wa miaka 25 ni mmojawapo. "Sisi ni mashujaa wanawake moyoni, kwasababu sio rahisi. sio kila mu anaweza kucheza mchezo huu. Inataka mazoezi mengi, na mwili huchoka," anasema.

Kabla ya mchezo kuanza hufanya tambiko kwa kuchoma na kufukiza matawi ya mti maalum.

Mchezo wa Ulama unaaminika kuwa tambiko za kitamaduni na kidini na wachezaji hii leo mjini Mexico huvaa mavazi maalum kufanya tambiko kabla ya kuingia uwanjani.
Huwakilisha mambo toafuati tukufu kama Mictlantecuhtli, Mungu wa wafu.

Mchezo huo umekubalika na wengi mjini Mexico baadhi ambao wanasema badala ya kuuokoa mchezo wa Ulama, mchezo huo umewaokoa wao kwa kufanikiwa kuwapa malengo mapya.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?