Tetesi za soka Ulaya Jumatatu tarehe 23.09.2019: Xavi, Keane, Mourinho, Balotelli, Sottil, Hysaj
Kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona Xavi, ambaye ni meneja wa timu ya Qatari ya Al-Sadd, anasema kuwa itakuwa ni tatizo kwake kuwaongoza wachezaji wenzake wa zamani kama vile Lionel Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets katika Nou Camp.
Kaeni nje ya Ghuba, Iran yaonya vikosi vya kigeniPicha: 'Sekunde kadhaa kabla ya ajali ya ndege'WHO lalalamika ukosefu wa ushirikiano kutoka Tanzania kuhusu Ebola
Tottenham imetuma ujumbe kumchukunguza mchezaji wa kimataifa wa timu ya vijana waliochini ya miaka 21 wa Italia winga wa Fiorentina Riccardo Sottil ambaye ni mchezaji wa kiwango cha juu huku wakionyesha nia ya kumchukua kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 .
Matumaini ya Chelsea ya kusaini mkataba na mchezaji wa Napoli Elseid Hysaj msimu ujao yanaweza kugonga mwamba huku klabu hiyo ya Italia ikiwa tayari kurefusha mkataba na kijana huyo kutoka Albania mwenye umri wa amiaka 25. (Express)
Meneja wa Everton Marco Silva ameutuma ujumbe umchunguze zaidi mshambuliaji wa timu ya RB Leipzig Yussuf Poulsen, mwenye umri wa miaka 25.
Maoni
Chapisha Maoni