Yanga wamlilia Manji

WANACHAMA wa Yanga wamemuangukia mwenyekiti wao aliyejiuzulu Yusuf Manji baada ya kukataa ombi la kuachia ngazi la kiongozi huyo. Wanachama wa klabu hiyo kutoka matawi 65 ya mkoa wa Dar es Salaam walikutana jana na kumtaka makamu mwenyekiti wao, Clement Sanga kuhitisha haraka kmkutano wa dharura.

Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, ambapo kwa pamoja waliazimia kukataa ombi la kujiuzulu kwa Manji. “Wanachama hawataki Manji akae pembeni, wanataka mkutano wa dharura uitishwe siku 14 toka leo kwa mujibu wa katiba, kamati ya utendaji inakaa leo ( Jana) mchana itapitia maombi ya wanachama na kutoa maamuzi.” alisema Mkwasa.

Naye Makamu Mwenyekiti wa matawi Bakili Makele alisema kuwa baada ya kutafakari barua ya Manji, ambayo inaeleza moja ya sababu ya kujiuzulu ni kutokana na afya yake, lakini wao wanasema bado wanamuhitaji.

Naye Mwenyekiti wa Keko Ukombozi Joseph Kalindwa akizungumzia hilo alisema “ Manji alitukuta kipindi kigumu mno tukiwa tumegubikwa na mgogoro wa Yanga Kampuni, Asili lakini aliweza kutusuluhisha na tukaa sawa.

Manji alitangaza kubwaga manyanga juzi akidai kuwa ni wakati muafaka kwa yeye kupumzika. “Nimeamua nipumzike nipishe wengine waongoze, Yanga ni yetu sote nilipngezewa muda tu kwa demokrasia lakini haimanishi kuwa Mimi ndio nitakua Mwenyekiti milele.” alisema Manji ambae hata hivyo si mara yake ya kwanza kutangaza kuachana na klabu hiyo.

Agosti mwaka jana pia alitangaza kujiuzulu ikiwa ni siku chache tangu alipotangaza kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka 10, huku asilimia 75 za timu hiyo zikiingia kwake na kutoa asilimia 25 kwa timu hiyo kila mwaka kitu kilichopingwa na wadau wengi wa Soka ikiwemo serikali.

Hata hivyo wanachama wa klabu hiyo walimpigia magoti na kumsihi asitishe azma yake hiyo ambayo alikubali kuendelea na uongozi hadi juzi Jumamosi alipotangaza rasmi kujiuzulu.

“Ikumbukwe Yanga ni klabu ya wanachama, Yanga ni kubwa kuliko mtu yoyote, naamini watakaofuatia wataendeleza pale nilipoishia.” alisisitiza. Hata hivyo kuondoka kwa Manji kunaweza kukawa si pigo sana kwa klabu hiyo ya Jangwani ambayo tayari imesaini mamilioni ya fedha kwa kudhaminiwa na SportPesa huku ikielezwa kuwa kuna makampuni kadhaa ambayo yapo mbioni kudhamini timu hiyo ya mtaa wa Jangwa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?