Asernal manager, Arsene Wenger aongeza mkataba mpya


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekubali kuchukua mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo, hatua itakayoendeleza muda ambao amekaa katika klabu hiyo.
Mfaransa huyo amekuwa meneja wa Arsenal kwa miaka 21 sasa.
Wenger na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke walikutana Jumatatu kuamua hatima ya meneja huyo, na kisha uamuzi wao ukawasilishwa kwa mkutano wa bodi Jumanne.
Arsenal wanapanga kutangaza rasmi uamuzi huo Jumatano.
Gunners walimaliza Ligi ya Premia wakwia nafasi ya tano, mara yao ya kwanza kumaliza chini ya nafasi ya nne tangu Wenger alipojiunga nao mwaka 1996.
Walimaliza alama 18 nyuma ya mabingwa Chelsea, lakini walifanikiwa kuwachapa Blues katika fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley Jumamosi.
Mkataba wa Wenger ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Wenger: Sitasoma kitabu cha Mourinho
Mourinho: Nafurahi mashabiki wa Arsenal walifurahi
Wenger aliongoza Gunners kushinda mataji matatu ya Ligi ya Premia na pia vikombe vinne vya FA misimu yake tisa ya kwanza kwenye usukani.
Mwaka 2003-04, aliibuka meneja wa kwanza tangu 1888-89 kuongoza timu iliyomaliza ligi kuu bila kushindwa.
Lakini baada ya kushinda Kombe la FA mwaka 2005, walisubiri kwa miaka mingine tisa - sawa na siku 3,283, kabla ya kushinda kikombe kingine.
Walilaza Hull City fainali ya Kombe la FA mwaka 2014 na kisha wakashinda kikombe hicho tena mwaka uliofuata.
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakimtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 67 ajiuzulu, hasa baada ya matokeo mabaya msimu huu. Shutuma zaidi zilitolewa waliposhindwa kwa jumla ya mabao 10-2 na Bayern Munich katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Machi.
Fans protesting against Arsene WengerHaki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Wenger amekuwa akitakiwa na baadhi ya mashabiki ajiuzulu
Walimaliza msimu wakiwa wameshinda mechi tano mfululizo, lakini matokeo hayo hayakutosha kuwawezesha kuwapita Liverpool waliomaliza nafasi ya nne na kujaza nafasi ya mwisho ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Jumamosi, Wenger aliambia BBC kwamba shutuma na uokosoaji aliokumbana nao msimu huu ni wa "kufedhehesha" na kwamba hatawahi kuusahau kamwe maishani

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?