Robert Mugabe akumbukwa kwa hotuba za ujasiri dhidi ya ukoloni:

Mugabe amefariki akiwa na miaka 95 huku akikumbukwa kwa ujasiri wake dhidi ya ukoloni kutokana na misimamo yake nchini Zimbabwe.

Baadhi ya maneno ambayo Mugabe aliyowahi kuyasema dhidi ya bara la ulaya kuhusua nchi yake.

"Zimbabwe ni huru kwa sababu watu wake wako huru na watu wake wanapaswa kuwa huru daima"

"Sisi sio watu wa ulaya, hatujawahi kuomba hata sehemu ndogo ya ulaya, Blair kaa na Uingereza yako na mimi niache nibaki na Zimbabwe yangu"

Awali Mugabe alisifiwa kwa kupanua sekta ya afya na elimu kwa weusi walio wengi, baadaye alitumia ghasia dhidi ya wapinzani wake na kuongoza uchumi wa taifa hilo ulioanguka vibaya.

"Hawawezi kuanzisha demmokrasia hapa, sisi tumeanzisha demokrasia"

"Hii ni ardhi ya mtu mweusi hivyo ni mtu mweusi ndio ana haki ya kuamua nani akae na nani asikae"

"Tuna ardhi yetu na katika ardhi yetu ndio tutapata fedha"

Kimataifa mpiganaji huyo wa zamani alionekana kama dikteta kufuatia hatua ya jeshi lake kuwashambulia wapinzani wake mbali na kunyakuwa ardhi kutoka kwa wakulima wachache weupe ili kupiga jeki umaarufu wake miongoni mwa wapiga kura.

Uongozi wake umezua mjadala mkubwa tangu kifo chake.

Alikuwa maarufu miongoni mwa wapiga kura wengi hata katika kipindi chake cha hivi karibuni alipong'atuliwa mamlakani.

Aliondolewa mamlakani alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa ambaye baadaye alikuwa rais wa taifa hilo.

Rais Emmerson Mnangagwana amempongeza Mugabe tangu habari za kifo chake zianze kutolewa.

Bwana Mnangagwa alisema kwamba chama tawala Zanu -PF kilimpatia hadhi ya ushujaa wa taifa aliyohitaji.

Hivi karibuni kuna madai kutoka upinzanini yalidai kuwa maisha ya Zimbabwe sasa ni magumu zaidi hata yalivyokuwa wakati wa utawala wa Robert Mugabe (hiyo ni kwa mujibu wa Fadzayi Mahere wa chama cha upinzani cha MDC).

Upande wa upinzani nchini Zimbabwe umewataka watu waandamane juu ya hali mbaya ya kiuchumi katika taifa hilo, serikali imeshutumiwa kwa kushindwa kufanya kazi yake.

Tangu mwaka 2017, Zimbabwe imekuwa chini ya utawala wa rais Emmerson Mnangagwa, baada ya jeshi kumuondoa kwa Robert Mugabe baada ya kutawala kwa kipindi cha muda mrefu .

Tumepima utofauti huo kwa kuangalia viashiria vya uchumi vya taifa vya maisha ya raia wa Zimbabwe kuwa wako kwenye hali mbaya sasa zaidi ya walivyokuwa kabla ya Mnangagwa kuingia madarakani.

Hii inaweza kuchukuliwa kama ufinyu wa ajira na mishahara kwani biashara imekuwa ya mashindano katika nyakati ngumu za kiuchumi.

Uchumi Zimbabwe ni mbaya kiasi gani?

Licha ya takwimu iliyokadiriwa ya mwaka 2019 iko chini kidogo ya ile ya 2017, amabayo ndio ilikuwa mwaka wa mwisho madarakani wa raisi Mugabe.

Pamoja na kuwa raia wa Zimbabwe wanaweza kuwa wanakabiliana na changamoto ya kushuka kwa takwimu hiyo ya hivi karibuni, si rahisi kujadili takwimu kutokana na hali kuwa mbaya zaidi hivi leo kuliko ya uongozi uliopita.

Hata hivyo, hatua nyingine muhimu haina budi kuchukuliwa juu ya hali ya uchumi ambayo ni hatua nyingine ya uwekezaji katika biashara.

Hakuna muda uliotangazwa kuhusu mazishi yake , huku mamlaka nchini Singapore ikishirikina na ubalozi wa Zimbabwe kuusafarisha mwili wake nyumbani.

Mugabe alikuwa akipokea matibabu nchini Singapore tangu mwezi Aprili.

Siku tatu za maombolezi ya kataifa zimeanza Zimbabwe kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa taifa hilo Robert Mugabe.

Mugabe ambaye ndio rais wa kwanza wa taifa hilo aliongoza taifa hilo hadi alipopinduliwa na jeshi 2017.

Licha ya kupinduliwa kwake , chama tawala Zanu- PF kimemtangaza kuwa shujaa wa kitaifa.

Je Robert Mugabe ni nani?

Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu

Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali

Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake

Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake

Uchumi ulidororeka baada ya mwaka 2000…

Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara ya uchumi

Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai

Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi

Ndoa yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza.

Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake.

Jeshi limeonesha kumtaka Emmerson Mnangagwa aliyefutwa kazi kama makamu wa Rais na Mugabe mwezi Novemba






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?