Swahiliflix kunadi filamu za kiswahili kimataifa

Katika jitihada za kukuza soko la filamu nchini Tanzania, wasanii nchini humo wameanzisha programu tumishi inayojulikana kama Swahiliflix, ikiwalenga zaidi wapenzi wa filamu hizi walioko maeneo mbalimbali duniani.

Waendeshaji wa programu hii tumishi wanahitaji filamu 14 kila juma lakini sasa wanapata fiilamu moja pekee yenye ubora.

Na katika kuinua ufanisi wa kazi hiyo waendeshaji wanakiri kuwa changamoto bado ni kubwa lakini wameanza jitihada kadhaa kuzifanyia kazi.

"Bado kuna changamoto katika uandaaji wa filamu za kiswahili lakini tuna mipango thabiti ya kuhakikisha kuwa na filamu zenye taswira zenye ubora zaidi na tuna uhakika baada ya muda mfupi swahiliflix itakuwa ni sehemu ambayo mtu akitaka kuangalia kitu chenye ubora wa juu anakuja kwetu"Maximilian Rioba ni mkurugenzi wa programu hiyo.

Hadi sasa zaidi ya watu elfu kumi na tano wameanza kufaidi matunda ya mfumo huo wa lugha ya Kiswahili ikiwa ni chachu ya kueneza lugha ya kiswahili.

Ni nani aliyeandika Kiswahili kibovu katika filamu za Netflix?

"Soko la filamu limetawaliwa na lugha ya kiswahili Afrika mashariki na kati"

Kwa muda sasa soko la filamu nchini Tanzania limekuwa likiporomoka lakini wadau wa filamu za Kiswahili wanasema huenda jukwaa hili likarejesha matumaini ,

"Tuna matumaini kuwa tunafikia kiwango cha kimataifa kutokana na filamu nilizoziona humo"

"Sio lazima kwenda kununua mkanda wa video au kuazima mikanda, popote nilipo ninaweza kuangalia filamu kwenye simu yangu au komputa na kufurahia sinema".

Wasanii wa filamu wanasema ujio wa programu hii ni mwanzo mpya na wanajizatiti kuwekeza Zaidi

"Watu walikuwa hawafanyi kazi zaidi kwa sababu walikuwa hawajui wanazipeleka wapi hizo filamu lakini sasa sehemu ya kuzipeleka ipo,"msanii wa bongo movie Raymond Kigosi aeleza

Huenda sasa jina Bongo Movie nalo likapenya kwenye rubaa za kimataifa na kuchuna vyema katika soko la filamu ulimwengun

Swahiliflix imeanzishwa wakati kampuni maarufu ya Netflix, inayotoa huduma za video mtandaoni moja kwa moja, imezinduliwa katika mataifa karibu yote duniani na kuzua msisimko mkubwa.

Sekta ya burudani pia haikuachwa nyuma katika kutumia Kiswahili hususan kupitia kutafsiri kazi zao kwa lugha hiyo ili kuwalenga takriban watu milioni 200 wanaoizungumza.

Kunao wanaoamini itatoa ushindani kwa zinazotoa huduma za runinga, filamu na video kwa malipo.

Wengi wanaitazama kama njia ya kuwawezesha kupata video, ambazo awali walikuwa hawawezi kuzipokea, kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Mahitaji ya lugha ya kiswahili yameongezeka duniani huku baadhi ya vyuo vikuu vikianzisha lugha hiyo pamoja na vitivo kamili.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?