Ubalozi wa Marekani: Hatutasita kuwachukulia hatua watakaovuruga au kukwaza demokrasia Tanzania

Ubalozi wa Marekani umesema kwamba haumuungi mkono mgombea yeyote au chama chochote katika uchaguzi ujao wa Tanzania.
''Tunaunga mkono mchakato wa kweli wa uchaguzi huru, wa haki na wenye uwazi, kabla, wakati na baada ya siku ya uchaguzi. Hii ni pamoja na usalama wa wagombea wote, kuheshimiwa kwa utawala wa kisheria na hali ya mamlaka na vyombo vilivyopewa wajibu wa kusimamia na kuendesha uchaguzi kutokupendelea kabisa upande wowote'', ulisema ubalozi huo.
Kupitia taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya ubalozi wa taifa hilo nchini Tanzania, ubalozi huo hatahivyo umesema kwamba utafuatilia kwa karibu matendo ya watu wanaoingilia na kuvuruga mchakato wa kidemokrasia au kuchochea vurugu dhidi ya raia.
Aidha ubalozi huo umesema kwamba unaunga mkono wito uliotolewa na wagombea wakuu wa kuwepo kwa mchakato wa uchaguzi wa amani na wenye uwazi.
''Tunatoa wito kwao na kwa wafuasi wao kuchukua hatua kutanzua hali ya usalama inayojengeka na kuepuka matamshi ya kichochezi'', ilionya taarifa hiyo.
Umesema kwamba uendeshaji wa chaguzi zijazo nchini Tanzania utakuwa na matokeo muhimu sio tu kwa Tanzania bali pia kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki.
Vilevile taarifa hiyo iliongezea kwamba historia ya Tanzania kuendesha chaguzi za amani imelifanya taifa hilo kuwa mfano wa kuigwa katika bara Afrika.
''Historia ya Tanzania ya kuendesha uchaguzi zinazohusisha vyama vingi inarudi nyuma hadi miaka 25 iliyopita na kuifanya nchi hii kuwa mfano wa Kuigwa katika bara hili', ilihitimisha taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.
Bado hakuna tamko lolote kutoka kwa chama chochote nchini humo baada ya tarifa hiyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?