Carlo Acutis, atununikiwa utakatifu wa digitali

Kanisa Katoliki limepata baraka mpya Oktoba 10, kwa namna ya kipekee mno : Mshawishi ambaye mwili wake umeoneshwa kwenye laba,jeans na sweta.

Leo hii Carlo Acutis anatangazwa kuwa mtakatifu katika mji wa Assisi, jimbo la Perugia, Italia.

Acutis alifariki akiwa na umri wa miaka 15 kutokana na kansa ya damu mnamo Oktoba 12, 2006.

Kijana huyo mdogo alijulikana sana katika jumuiya wa wakristo kutokana na kazi aliyoifanya katika kanisa kwa kutumia teknolojia mpya , kwa mujbu wa taarifa kutoka Vatican.

Acutis alizaliwa mjini London mwaka 1991, ambako wazazi wake walihamia kwa ajili ya kazi lakini alikulia Milan.

Acutis anatunukiwa utakatifu mapema sana tofauti na watakatifu wengine waliopita, ni baada ya miaka 14 tu tangu kifo cha kijana huyo.

Acutis ni mwenye heri wa kwanza wa "millenia hii " aliyetumia mtandao kutumika katika kanisa, aliyeonesha mfano wa teknolojia inavyoweza kutumika vizuri sana katika kanisa.

Hivi ndivyo Papa Pope Francis mwenyewe alivyomuelezea , kwa kusema kuwa kijana huyo mdogo alijua jinsi ya kutumia teknolojia ya mawasiliano mapya katika kuhubiri neno la Mungu, kuwasilisha maadili na uzuri wa kumtukuza Mungu."




Wakatoliki wengi wanamchukulia kama Msimamizi au Mtakatifu wa mtandaoni kutokana na kujitoa kwake katika kuongea kuhusu imani yake na kusaidia wengine katika teknolojia.

Acutis alikuwa ni mfano wa imani kwa vijana wadogo.

Carlo Acutis alitumia intaneti kusambaza imani ya kanisa katoliki kwa namna mpya.

"Kwa umri wake mdogo alikuwa katekista, aliweza kufundisha watoto wadogo imani ya kikristo na sio kwa kukutana tu kama ilivyozoeleka, yeye alitumia intaneti," Kadinali Becciu anafafanua.

" Alianzisha mradi wa komputa katika masuala ya imani, alisema miujiza ya Ekaristi. Hivyo kijana huyu mdogo aliishi maisha ya imani sana," aliongeza kusema kadinali.Miujiza ya Acutis

Kanisa lilimtangaza kuwa mwenye heri Julai 5, 2018, na kuainisha miujiza aliyoifanya: Mwaka 2013 alimuokoa mtoto mmoja raia wa Brazil ambaye alikuwa na ugonjwa wa nadra sana kutokea.

Familia ya mtoto huyo kujumuika naye katika sala yake mtandaoni.

Mtoto huyo wa kiume aliyezaliwa mwaka 2010 huko Campo Grande, Brazil, alikuwa anahitajika kufanyiwa upasuaji.

Lakini alipona kabla ya kufanyiwa upasuaji baada ya kufanyiwa maombi maalumu na maneno aliyoyaacha mtandaoni Carlos.

Uponyaji wake ni sababu ya kutambuliwa kuwa mtakatifu kutokana na miujiza muhimu mbalimbali iliyowatokea watu kutokana na kazi yake.

Kwa upande mwingine, mwili wake ambao ulikuwa umetunzwa umeonyesha kufanya miujiza mingi mipya hivi karibuni.

Ingawa kanisa limefafanua kuwa mwili wake haukupatikana ukiwa haujaharibika.

Wakati ambao mwili wake ulihamishwa mwaka 2019 katika makaburi ya Assisi, mwili huo ulitunzwa vizuri 

.Follow us on Instagram

Follow us on Facebook

Follow us on Twitter

Subscribe our YouTube channel






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?