Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 01.10.2019:Sancho, Vertonghen, Mandzukic, Alderweireld, Wenger
Kocha wa zamani wa Arenal, Arsenal Arsene Wenger yupo kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa na miamba ya Italia AC Milan kurithi mikoba ya kocha Marco Giampaolo. Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 21, anatarajiwa kukataa ofay a kuchezea timu ya taifa ya Nigeria na badala yake kuelekeza nguvu zote kwa England iwapo ataitwa na kocha Gareth Southgate katika michezo ya kufuzu Euro 2020 dhidi ya Jamhuri ya Czech na Bulgaria. Mkurugunzi wa michezo wa Borussia Dortmund amefichua kuwa hadhani kuwa nyota wao kinda Jadon Sancho, 19, akisalia klabuni hapo kwa muda mrefu. Sancho kutoka England alikuwa akihusishwa na Man United katika dirisha la usajili lililopita. Beki wa Manchester United na timu ya taifa ya Ivory Coast Eric Bailly sasa kusalia nje ya uwanja mpaka mwezi Januari. Baily, 25, alipata majeraha ya goti kwenye mchezo wa kujiandaa na msimu dhidi ya Tottenham. Beki wa Tottenham Jan Vertonghen, 32, ambaye makataba wake unaisha mwishoni mwa msimu amesema kuwa anaw...