Trump aiomba China kumchunguza mpinzani wake

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye tayari anakabiliwa na shutuma inayoweza kumuondoa madarakani baada ya kumtaka rais wa Ukraine kumchunguza mpinzani wake Joe Biden, na sasa inasemwa kuwa aliwatakata China wafanye vivyo hivyo.

Aliziambia nchi zote mbili, China na Ukraine kumchunguza bwana Biden ambaye ni kinara wa chama cha Democratic anayetaka kuwania urais, na mtoto wake.

"China inapaswa kuanza kumchunguza Biden," alisema Trump.

Democrats imemshutumu rais Trump kwa madai ya kutoa msaada wa kijeshi kuwa njia ya kumfanya aweze kuibua mabaya ya bwana Biden.

Bwana Biden alijibu kupitia ukurasa wake wa tweeter kuwa Trump ana wazo la kumshambulia mtu yeyote mwenye msimamo ni utani.

Mazungumzo ya simu kati ya rais Trump na kiongozi wa Ukraini rais Volodymyr Zelensky,Julai 25 yalipelekea wapelelezi kupeleka taarifa zinazoweza kumuondoa Trump madarakani.

Ingawa siku ya alhamisi, rais Trump alidai kuwa madai hayo ni upuuzi.

Katika ujumbe wake wa usiku wa manane kupitia kurasa yake ya Tweeter, Trump aliongeza kuwa yeye ana jukumu la kuchunguza kashfa za rushwa, jambo ambalo linajumuisha na kuuliza na kutoa mapendekezo kwa nchi jirani kutoa msaada.

Trump anamshutumu bwana Joe Biden na mtoto wake Hunter kwa kashfa za rushwa katika mikataba yao ya kibiashara na kisiasa nchini Ukraine na China , bila ya kutoa ushaidi wa kuthibitisha madai yake.

Wakati ambao Hunter Biden alipoingia katika mkataba wa gesi asilia katika katika kampuni ya Burisma mwaka 2014, maswali mengi yaliibuka kuwa anaweza kuleta mgogoro kisiasa na baba yake.

Ukraine ilikuwa inakabiliana na mgogoro wa kisiasa baada ya kiongozi wake kulazimishwa kuondoka madarakani, huku Biden alikuwa katika ngazi za juu za utawala wa Obama.

Mwaka 2016, Joe Biden aliisukuma serikali ya Ukraini kumfukuza mwendesha mashitaka Viktor Shokin, ambaye ofisi yake ilikuwa inaichunguza kwa karibu mmiliki wa kampuni ya Burisma.

Katika hotuba yake mwaka jana bwana Biden alijisifia kwa kumfukuza bwana Shokin na kutishia kutotoa mkopo wa mamilioni ya fedha kwa Ukraine.

Bwana Trump na washirika wake wanamshutumu bwana Biden kwa kumlinda mwanae.

Hata kama maafisa wengine wa serikali ya Ukraine pia walitaka bwana Shokin kuondoka madarakani kwa sababu ya jitihada zake za kukabiliana na rushwa.

Wiki iliyopita mwendesha mashtaka nchini Ukraini ambaye alichukua wadhifa wa bwana Shokin aliiambi BBC kuwa hakuna ushaidi wa uovu alioufanya bwana Joe au Hunter Biden.


Trump alpohojiwa kuhusu mazungumzo yake ya simu na rais wa Ukraini bwana Volodymyr Zelensky alijibu kuwa jibu ni rahisi kuwa ;

"Nilidhani kuwa wameanza kufanya uchunguzi tayari kama kweli walikuwa na nia njema basi wangeanza kumchunguza Biden,"

"Wanapaswa kumchunguza Biden" alisema Trump wakati alipohojiwa na waandishi wa habari katika ikulu ya Marekani.

"Vilevilevile, China pia inapaswa kuanza kumchunguza Biden kwa sababu kile kilichotokea China ni sawa na kile kilichotokea Ukraine", Trump aliongeza.

Trump alipendekeza tena bila kutoa ushaidi wowote dhidi ya Biden na kwa kudai uhusiano wa kibiashara kati ya Biden na mataifa hayo mawili, China na Ukraine .

Mkuu wa tume ya uchaguzi aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter kuwa ni kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kuhusisha madai ya nchi za kigeni katika uchaguzi wa Marekani.


Biden ametoa majibu gani?

Msemaji wa bwana Biden wa kampeni za mwaka 2020 amemshutumu Trump kwa kutumia vibaya televisheni ya taifa kwa taarifa za kusadikika.

Naye msemaji wa Hunter Biden ameviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa kiwango cha dola bilioni 1.5 ni hesabu ya uongo, hawawahi kupokea fidia yoyote ya malipo ya kiwango hicho cha fedha katika kiwanda chochote China.


Bidens alifanya nini China?

Mwaka 2013, bwana Biden alipokuwa makamu wa rais alipofanya ziara ya kiofisi nchini China na kukutana na rais wa nchi hiyo Xi Jinping.

Hunter Biden na binti yake waliongozana naye.

Biden alikuwa makamu wa rais wa kwanza kuongozana na familia yake katika shughuli za kikazi.

Katika ziara hiyo ya siku mbili , Hunter alikutana mfanyakazi wa benki wa nchini humo, Jonathan Li, ambaye baadae akawa mshirika wake katika biashara.

Bwana Li alipata ufadhili binafsi muda mfupi tu baada ya ziara hiyo ingawa msemaji wa Hunter alikiambia chombo cha habari cha NBC News kuwa hawakujadili masuala yoyote ya kibiashara katika ziara ile na ufadhili ulikuja miezi michache baadae.

Hunter amekanusha kuwa na mkutano wowote kuhusu biashara na afisa wa China.


Athari za uchunguzi dhidi ya Trump

Uhalifu anaoshutumiwa nao Trump unaweza kumuondoa rais madarakani, na unapitia hatua mbili za mchakato wa kisiasa.

Kama kura za wawakilishi hazitatosha, basi bunge la seneti litalazimika kusimamia kesi hiyo.

Kura ya seneti inahitaji walau wingi wa theluthi mbili ya wingi - na inaweza kushindwa kwa sababuchama cha Trump kina maseneta wengi zaidi.

Ni marais wawili tu katika historia ya Marekani ambao ni Bill Clinton and Andrew Johnson ambao walikabiliana na kesi ya namna hiyo na hakuna kati yao ambaye alishtakiwa au kuondolewa madarakani.

Rais Nixon alijiondoa madarakani kabla ya kung'olewa na bunge.

.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?