Rais Magufuli atangaza kuhamia Dodoma rasmi

Rais wa Tanzania , John Pombe Magufuli ametangaza kuhamia rasmi katika mji mkuu wa taifa hilo, Dodoma.

Rais Magufuli anakuwa rais wa kwanza kati ya marais watano waliotawala nchi hiyo , kutekeleza uhamisha wa makao makuu ya Tanzania kutoka jiji la kibiashara la Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Uhamisho wa makao makuu ya serikali mkoani Dodoma, umechukua safari ya zaidi ya miaka 42 iliyopita.

Rais Magufuli alitoa amri ya serikali kuhamia Dodoma mwezi Julai 2016 wakati alipopewa wadhifa wa mwenyekiti wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi.

Ambapo waziri mkuu alianza kuhamia katika mji huo na kufuatia na viongozi wengine pamoja na wizara tangu mwaka 2016.

Magufuli alidhihirisha hilo hapo jana ,12.10.2019 kwa kujiandikisha katika katika daftari la orodha ya wapiga kura katika kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma.

Chamwino ni eneo ambalo, ikulu mpya ya rais iko.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alihamia rasmi mji wa Dodoma septemba 26, 2016.

Umbali wa mji wa Dar es Salaam mpaka Dodoma ni takribani kilomita 450.

Kwa muda wa miezi minne sasa ofisi za serikali zimekuwa zikihamishwa kwenda mji wa Dodoma.

Shughuli hiyo ya kuhama inatarajiwa kuchukua miaka mitano na kugharimu dola milioni 500.

Dodoma ulitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania na mwasisi wa taifa hilo mwalimu Julius Nyerere mwaka 1973.

Sanamu la Mwalimu Nyerere lililopo mjini Dodoma limekuwa kuvutio kikubwa mjini humo hasa kwa vijana na wageni ambao mara nyingi huenda kupiga picha za ukumbusho

Tangazo la Rais Magufuli la kuhamishia serikali Dodoma ilikuwa na mtazamo tofauti tofauti , wengi wakiwa na hofu juu ya shughuli za na familia zao.

Huku wenjeji ikiwa fursa kwao na kuibua msisimko mpya na matumaini kwa wafanyabiashara.

Majumba makubwa na ya kifahari yanaendelea kujengwa katika mji huo.


Lakini changamoto kubwa ya mabadiliko hayo bado ikiwa ni kwa watumishi wa umma ambao inawabidi kufunga safari kila wakati kwa ajili ya familia zao.

Aidha wengi kuona mpango huu umeathiri familia zaidi katika ndoa na maendeleo binafsi.

Huduma muhimu za afya na shule , bado wananchi wana matumaini sekta nyingi binafsi zitaamia katika mji huo.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Watalii wa Ufaransa kukabiliana na hukumu ya wizi wa mchanga