Robert Kyagulani maarufu Bobi Wine asema Museveni anaongoza 'kwa mtutu wa bunduki'

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amemjibu rais Yoweri Museveni ambaye katika mahojiano na Newsday Swahili alimtaja kuwa adui wa maendeleo nchini humo.

Bobi Wine ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulani , hivi majuzi alitangaza kwamba atamkabili bwana Museveni mwenye umri wa miaka 75 katika kinyanganyiro cha urais katika uchaguzi wa 2021.

Rais huyo wa Uganda amekuwa madarakani tangu 1986.

Bobi Wine atangaza azma yake ya kuwania urais UgandaMwandani wa Bobi Wine afariki Uganda

Katika ujumbe wake wa twitter Bobi Wine alimtaja rais huyo kuwa adui wa Uganda ambaye anaongoza kupitia 'mtutu wa bunduki'.

Katika mahojiano hayo ya Newsday Swahili , bwana Museveni alidai kwamba msanii huyo wa muziki alikuwa amesema katika ziara yake Marekani kwamba watu hawafai kwenda Uganda na kuwekeza.

Lakini mgombea huyo wa urais alisema kwamba Museveni huenda amekuwa akiota ndoto kwa kuwa hajawahi kutoa matamshi kama hayo.

Katika taarifa ambayo alisema huenda rais huyo alikuwa akizungumzia mnamo mwezi Septemba 2018 katika mahojiano na Al jazeera, alisema kwamba ''Wamarekani wanafaa kuwa na wasiwasi wa kumpatia Museveni ufadhili wa kijeshi kwa kuwa ufadhili huo hautumiki kuwalinda raia wa Uganda''.

Bwana Museveni anataka kugombea muhula wa sita kama rais mnamo mwaka 2021 baada ya kuwa rais wa nchi hiyo kwa miaka 33.

Bobi Wine, ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la 'The People Power', anamshutumu rais huyo kwa kuongoza kwa mfumo wa ukandamizaji.

Bwana Museveni amekataa kumueleza mwandishi wa Newsday Swahili , Alan Kasujja ikiwa serikali yake ni ya ukandamizaji , lakini akasema anamshughulikia Bobi Wine kama adui.

Rais huyo wa Uganda amemlaumu Bobi akisema kuwa alikwenda Marekani na kusema kwamba watu wasije kuwekeza Uganda: ''Unapokwenda na kuwaambia wageni kwamba hawapaswi kuja na kuwekeza katika nchi yetu, inamaanisha umeanzisha vita dhidi ya mafanikio yetu. Kwa hiyo kwa nini sasa unataka kurejea na kunufaika na mafanikio hayo?".
Hii huenda ndio moja ya sababu za kufutwa kwa matamasha ya muziki ya Bobi Wine, bado sijaongea na polisi kupata taarifa zaidi, alisema.
Rais huyo wa Uganda anasema bado ataendelea kuwepo madarakani kwa miaka mingine zaidi kukamilisha kile ambacho yeye binafsi na wapiganaji wenzake walikipanga kukifanikisha katika nchi yao na Afrika.

''Nyumba yangu inanisubiri, lakini tuna masuala kama Uganda ya kushughulikia. Ni masuala hayo ambayo yanatufanya tufanye kile tunachotaka kukifanya kisiasa pamoja na wenzetu. Kama chama tawala (NRM) kitafikiria kuwa hakihitaji mchango wa wazee basi tutaondoka madarakani kwa furaha na kufanya mambo mengine ." Museveni alimueleza mwandishi wa Newsday Swahili Allan Kasujja mjini Kampala.

''Hatupo hapa kwa ajili ya maonyesho, hatuendi kwenye ukumbi wa michezo ya maigizo , sisi ni watu ambao tupo hapa kushughulikia emasuala makubwa ya Uganda na Afrika ." Alisistiza kiongozi huyo wa Uganda.

Bobi Wine ameonyesha kukerwa na kauli ya Museveni kuwa yeye ni adui wa maendeleo.

Rais Yoweri Museveni amekuwa madarakani Uganda sasa kwa zaidi ya miongo mitatu.

Bwana Museveni amekuwa akikabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu hasa kutoka kwa vijana na wapinzani wake .

Mpinzani wake wa muda mrefu Dkt Kizza Besigye amepitia misukosuko mingi katika harakati zake za kisiasa pamoja na Mbunge Bobi Wine ambaye juhudi zake za kutumia usanii wake wa kimuziki kuhimiza ajiuzulu zimekuwa zikizimwa na maafisa wa usalama.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?