Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 07.10.2019: Solskjaer, Boly, Gerrard, Kane, Kante, Wilson, Pulisic

Makampuni ya kamari yameongeza dau juu ya uwezekano wa kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kufutwa kazi baada ya kukubali kichapo cha kushtukiza dhidi ya Newcastle. Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anapigiwa upatu kuchukua mikoba ya Solskjaer. 

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kuwa mrithi wake klabuni hapo atakuwa kocha wa Rangers ya Uskochi Steven Gerrard ama kocha wa zamani wa klabu hiyo forme Kenny Dalglish.

Gerrard na Dalgish wote wameichezea Liverpool kwa mafanikio makubwa. 

Beki wa zamani wa Liverpool Glen Johnson amemshauri mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 26, tkuihama klabu yake na kumpigia chapuo ajiunge na Man City. 

Kocha wa Arsenal Unai Emery anapiga hesabu za kumnunua beki wa Wolves Willy Boly. Wolves wanaweza kutaka dau la pauni milioni 20, wao walimnunua nyota huyo raia wa Ivory Coast kwa pauni milioni 10. 

Winga wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs anaamini Ole Gunnar Solskjaer anatakiwa kusajili wachezaji wengine watano ili timu irejee kwenye kiwango chake. (Sun

Real Madrid wapo tayari kuchuana na Juventus ikatika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili kiungo mkabaji wa Chelsea N'Golo Kante. Vigogo hao wa La Liga wanaweza kulipa dau la uasajili la kufikia pauni milioni 70 ili kumnasa Mfaransa huyo. 



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?