Mama Martha Anne-Bowre: Ayaokoa maisha ya wasichana dhidi ya uavyaji mimba kwa kushinikiza umuhimu wa afya ya uzazi

Uavyaji mimba ni kinyume cha sheria katika baadhi ya mataifa barani Afrika jambo ambalo limekuwa likichangia wasichana na hata wanawake kutafuta njia za siri na ambazo ni hatari kulitekeleza hilo.

Martha Anne Bwore mwanaharakati anayepinga uavyaji mimba nchini Kenya aliye na miaka 55 anaeleza huchangia hofu na mahangaiko wanayopitia wasichana wakati wanapoachwa bila mawaidha au muongozi sahihi kuhusiana na afya ya uzazi na tendo la ndoa.

Na ni jambo ambalo binfasi analifahamu kwa uzito, kutokana na kuipitia hali kama hiyo na kuishia kuavya sio mimba moja wala mbili, lakini saba.

Kilichomshinikiza, anaeleza ni matamanio ya kupata mpenzi wa kuishi naye, kwani wapenzi aliobahatika kuwa nao walishinikiza kuavya mimba ili kuendeleza mahusiano hayo.

Uhuru wa maisha kwa mara ya kwanza

Bi Martha anasema alilelewa na wazazi waliokuwa wakali ambao hawakumruhusu hata kutoka nje.

Suala la ngono au mahusiano ni mambo ambayo yalikuwa mwiko kujadiliwa katika familia yake.

Uhuru wa maisha aliuonja kwa mara ya kwanza nchini India alikokwenda kusoma akiwa na umri wa miaka 17.

Hapakuwa na mzazi wala mlezi yeyote aliyekuwa akimfuatilia tabia zake.

Nikiwa India nilikuwa na hela , pombe , wanaume wapenzi na uhuru. Kisha hakukuwa na wingi wa warembo kwa hio tulichukuliwa kama malkia ," alisema Bwore .

Ni katika mishe hizo za maisha ndipo Martha aligundua kuwa alikuwa mja mzito kwa mara ya kwanza.

Kutokana na shinikizo la masomo aliamua pamoja na mpenziwe wakati huo kuiavya mimba.

India ni mmojawapo wa nchi ambazo zinasheria inayoruhuhusu uavyaji mimba.

Haikuchukua muda kabla ya Bowre kuendelea na maisha yake ya anasa na muda sio muda akajipatakwa mara nyingine katika hali ile ile ya kupata mimba nyengine.

Nilipomwambia mpenzi wangu kuwa nimeshika mimba alisema kuwa niiavye kwa kuwa tulikuwa bado vijana mimi ni yule mtu nikipenda naweza kufanya chochote kwa hio niliamua kuavya ."

Lakini haikuchukua muda kwa yeye kupata mimba kwa mara nyengine lakini hio ilikuwa kwenye mishipa ya njia ya mayai ya mwanamke hivyo basi mimba yenyewe ilitoka kwa kuwa daktari alimwambia ikingehatarisha maisha yake .

Baada ya mimba hiyo ya tatu, alianza kuwa na msongo wa mawazo na hapo alikunywa pombe kwa wingi na pia kujihusisha na ngono ikiwa ndio njia aliyoiamini ya kuyaondoa mawazo.

Miaka miwili baadaye 'nilishika mimba ya nne'.

Mpenzi wake wakati huo alimshurutisha aavye mimba licha ya kuwa yeye alitaka iwe siri ili awe mama. lakini mpenzi wake alipogundua ilimbidi aivye.

Pacha walioibadili roho

Martha anasema alipata mpenzi mwengine akiwa India na haikuchukua muda kabla yeye kushika mimba. Kama ilivyokuwa ya wapenzi wake wa awali, hata huyu alimshurutisha aavye mimba.

"Hii mimba ilikuwa ya miezi 5. Nilimweleza daktari kuwa nilitaka kuavya mimba , lakini daktari alinishauri nipigwe picha ya mimba kabla ya kuitoa na hapo iligundulika nilikuwa nimebeba mapacha ."

"Baada ya siku mbili za uchungu kupitia sindano nilizodungwa ili mimba itoke kwa uchungu niliwatizama mapacha wangu Kijana na Mischana wakiwa wamekumbatiana baada ya kutoka, nililia saana na kumuomba Mungu msamaha na hapo niliapa kutotoa mimba tena ," Bwore alisema .

Haikuchukuwa muda kabla ya yeye kushika mimba nyengine lakini wakati huu aliamua kuwa angezaa mtoto iwe atakuwa na mpenzi au la .


Marie Stopes yazuia huduma za uavyaji wa mimba Kenya

Matokeo ni kuwa Bwore ana watoto wawili, Msichana mwenye umri wa miaka 27 hii leo aliyemzaa akiwa bado masomoni huko India na Mvulana aliye na miaka 21 aliyemzaa baada ya kurejea nchini Kenya.

Kwa sasa Bwore ni mmoja wa watu wanaopinga uavyaji mimba.

Anajishughulisha kutoa ushauri kwa wasichana ambao wamefika mwisho na wanaotamani kutoa mimba hadi wakati ambapo wana imarika kimawazo.

Japo anajutia saana msururu wa mimba alizozitoa, anapania kutumia hali yake kama njia ya kuhamasisha umma dhidi ya hali hii ambayo inasema haifai.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?