Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 21.10.2019: Sancho, Haaland, Werner, Meunier, Koeman

Real Madrid inawafuatilia winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19 na mshambuliaji wa Norway wa miaka 19- Erling Braut Haaland, anayechezea Red Bull Salzburg. 

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig Timo Werner,23 ambaye aliwahi kuhusishwa na tetesi za kujiunga na Liverpool. 

Manchester United inajiandaa kumpatia mkataba mpya kiungo wa kati wa Uingereza Angel Gomes, 19, licha ya tetesi kuwa Barcelona inamtaka. 

Newcastle United inamfuatilia mshambuliaji wa Lille na Nigeria wa miaka 20 Victor Osimhen. 

Meneja wa Chelsea Frank Lampard anataka mshamsmbuliaji wa Ufaransa wa miaka 33, Olivier Giroud, ambaye hajafurahishwa na hatua ya kutojumuishwa katika kikosi cha kwanza aendelee kusalia Stamford Bridge. 

Chelsea imemuongeza aongeza mchezaji wa safu ya kati wa Atalanta na Ukraine Ruslan Malinovskyi, 26, katika orodha ya wachezaji amabao huenda wakahamia klabu hiyo msimu ujao wa joto. 

Beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 28, anasema angelijiunga na Everton msimu huu lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hakuridhishwa na ofa aliotolewa na klabu hiyo. 

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 28, anapanga kurejea katika ligi kuu ya ya England baada ya kupona jereha la mguu katika mechi ya klabu hiyo dhidi ya Sheffield United siku ya Jumatatu. 

Meneja wa Uholanzi Ronald Koeman angependelea kuwa msimamizi wa klabu ya Barcelona siku moja na anasema kuwa mkataba wake una kifungu cha sheria kinachomruhusu kuajiriwa na baada ya mashindano ya Ulaya mwaka 2020, amesema mkurugenzi wa michezo wa shirikisho la kandanda la Uhuolanzi, Nico-Jan Hoogma.

Tetesi Bora Jumapili

Manchester City inajiandaa kumlipa Raheem Sterling kitita cha £450,000-kwa wiki ili kukatiza azma ya Real Madrid ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Uingereza wa miaka 24. 

Paris St-Germain itamenyana na Real Madrid kujaribu kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?