Msako wa kuwakamata na kuwafunga walevi wanaoendesha magari unaendelea

Polisi nchini Rwanda inaendela na msako usio wa kawaida kuwakamata wanaoendesha magari huku wamelewa.

Katika kipindi cha takriban mwezi mmoja watu zaidi ya 700 wamekamatwa na kutiwa kufungwa , huku baadhi yao wakidai walionewa.

Polisi inadai kuwa kamata kamata hiyo ni sehemu ya kampeni ya muda mrefu yenye lengo la kupunguza idadi ya ajali za barabarani, hususan baada ya kubaini kuwa nyingi kati ya ajali hizo husababishwa na madereva wanaoendesha gari wakiwa walevi.

Licha ya kulipa fidia ya franga za Rwanda laki moja na nusu hivi sasa mwenye kubainika na kosa hilo pia hufungwa siku tano.

Wanaokamatwa hata hivyo wanadai kuwa mara nyingi huwa wapo wanaoonewa kwani njia ya inayotumiwa kubaini ikiwa mtu kweli ni mlevi ina utata.

Polisi nchini Rwanda inasema kuwa katika kipindi cha wiki mbili za mwisho wa mwezi wa Septemba watu 191 walikamatwa wakiwa ni walevi wa kupindukia, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa polisi kiwango cha 0'08 cha kileo katika damu ndicho kinachokubalika kwa mtu anayeendesha gari nchini Rwanda . Kiwango cha kileo mwilini hupimwa na kifaa kinachofahamika BAC na hupima kulingana na uzito wa mtu aliyekunywa pombe.

Wanaokamatwa wanadai kuwa unapokamatwa, polisi huwa hawawezi kukuonyesha kipimo chenyewe ili uangalie kama kweli umekunywa pombe kupita kiwango kinachotakikana.

Mmoja wa watu waliokamatwa na kufungwa siku tatu ambaye hakupenda jina lake litajwe , anasema kuwa kampeni hii ni kali na ina uonevu.

Anadai kuwa polisi hawatofautishi kunywa na kulewa, akisema kuwa alikamatwa akiwa amekunywa chupa tatu za pombe aina ya mutziig, kiwango ambacho amekuwa akinywa na kuendesha gari kama kawaida.

Licha ya Uretse imikwabu yakajijwe na polisi mu mihanda yo mu mijyi mu Rwanda, muri ubu bukangurambaga polisi inakurikirana cyane abacuruza inzoga bashobora kuziha abatagejeje ku myaka 18.

Katika baa nyingi yamewekwa matangazo yanayowakumbusha watu wasiendeshe magari wakati wamekunywa pombe.

Wamiliki wa baa nao wameagizwa kuwakumbusha na kuwaonya wateja wao pale wanapowaona wanabugia pombe kwa kiwango cha juu.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?