Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 16.10.2019: Kante, Mandzukic, Giroud, Bale, Mourinho

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86 kwa Mcolombia James Rodriguez mwenye umri wa miaka 28 anayecheza safu ya kati ili kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Chelsea Mfaransa N'Golo Kante.

 Desmarque, via Sport buliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 33, anasakwa na Manchester United lakini ameonywa kuwa atahitaji kushusha kiwango cha madai yake ya mshahara.

Hata hivyo Manchester United wanahofu kuhusu ugumu wa kusaini mkataba mpya wowote na wachezaji wapya katika kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari .

Kocha wa Arsenal Unai Emery hatazamii kupanua kikosi chake mweizi Januari wakati wa kipindi cha uhamisho wa wachezaji. 

Tottenham wameimarisha haja yao ya kumtaka Jose Mourinho huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu msimamo wa Manchester United wa kumtaka Mauricio Pochettino. 

Mshambuliaji wa Chelsea Mfaransa Olivier Giroud,mwenye umri wa miaka 33, anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo mwezi wa Januari ikiwa hatacheza tena. Inter Milan na timu ya Ligi kuu ya Canada Vancouver Whitecaps ni miongoni mwa timu zinazomtaka.

Mchezaji wa safu ya kati wa Croatia Luka Modric amemuomba mchezaji mwenzake katika kikosi cha Real Madrid Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 30, akimtaka abakie katika klabu baada ya mshambuliaji huyo wa kati wa Wales kukaribia kabisa kuhamia Bernabeu msimu uliopita. 

Kiungo wa kati Mbrazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27, bado anaweza kurudi Liverpool - ikiwa Bayern Munich wataaamua kutosaini mkataba wa kudumu na yeye msimu ujao . Kwa sasa anacheza kwa mkopo katika timu hiyo ya Ujerumani kutoka Barcelona. 

Paul Ince, ambaye ni nahodha wa kwanza mweusi wa England, anasema angewaongoza wachezaji wenzake kuondoka nje ya uwanja kama angekuwa anacheza katika mchezo baina ya Bulgaria na England Jumatatu ambao ulitawaliwa na matusi ya ubaguzi wa rangi .


Crystal Palace wanamtaka mshambuliaji wa safu ya kati wa Inter Milan Gabriel Barbosa, mwenye umri wa miaka 23, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Flamengo nchini Brazil. 




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?