Rais John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko serikalini

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi kadhaa serikalini huku akiwapiga kalamu viongozi wengine.

Kulingana na taarifa iliotoka katika Ikulu ya Tanzania na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Ikulu ya rais, walioteuliwa ni Mathias Kabunduguru ambaye sasa ndiye mtendaji mkuu wa mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Hussein Katanga aliyeteuliwa kuwa balozi.

Wengine walioteuliwa ni Godfrey Mweli kuwa naibu katibu mkuu Tamisemi anayeshughulikia elimu.

Kabla ya uteuzi huo Mweli alihudumu kama mkurugenzi wa mipango katika wizara ya katiba na Sheria.

Hashim Abdallah Komba naye ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Nachingwea. Kabla ya Uteuzi huo Komba Komba alikuwa akihudumu kama katibu tawala mkoa wa Iringa.

Anachukua nafasi ilioachwa na Rukia Muwango ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Vilevile kiongozi huyo wa taifa amemteua Hassan Abbas Rungwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Nachingwea. Anachukua mahala pake bakari Mohammed Bakari ambaye ameondolewa na huenda akapatiwa kazi nyengine.

Licha ya kwamba hakutoa sababu za kuwapiga kalamu maafisa hao, akiwa ziarani mkoani Lindi aliwaonya viongozi hao kwa kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo kulingana na gazeti la mwananchi nchini Tanzania.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?