Mrusi aishtaki Apple kwa kumgeuza kuwa mpenzi wa jinsia moja.

Mwanaume mmoja wa Urusi amewasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya kampuni ya vifaa vya kielekroniki Apple, akidai kuwa programu ya iPhone ilimgeuza kuwa mtu anayeshiriki mapenzi wa jinsia moja.

Anayasema hayo baada ya tukio jingine linalohusisha programu ya malipo ya ya kimtandao ya GayCoin yanayohusishwa na wapenzi wa jinsia moja.

Anasema alipata madhara sana ya kihisia na anadai alipwe pauni 12,000, kwa mujibu wa nakala ya mashtaka iliyolifikia shirika la habari la AFP.

Wakili wake , Sapizhat Gusnieva, anasema kuwa mteja "ana hofu kubwa, na anaumia ", na kuongeza kuwa kesi yake iliyowasilishwa mjini ni Moscow ya "uhakika".

Ni nini kilichotokea?

Katika mashtaka yaliyowasilishwa tarehe 20 Septemba, inadaiwa malipo ya biashara za mtandaoni yanayohusishwa na wapenzi wa jinsia moja "GayCoin" yalilipwa kupitia programu ya smartphone, kinyume na mfumo wa Bitcoin aliokuwa ameutumia kuagiza bidhaa.

Msalipo ya Crypto-currency hutumia pesa - ni aina ya pesa zinazotumiwa kwa ajili ya mtandao- na Bitcoin na GayCoin ni baadhi ya pesa za aina hiyo.

Kwa mujibu wa mlalamikaji pesa za GayCoin crypto-currency zilimfikia zikiwa na umbe unaosema : "Usihukumu bila kujaribu".

" Nilifikiria, kiukwelii , ni kwanini nihukumu kitu bila kukijaribu ? Niliamua kujaribu mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja ," uliandikwa waraka wa mashtaka ya Mrusi huyo.

"Sasa nina mpenzi wa kiume na sasa sijui jinsi ya kuwaelezea hili wazazi wangu."

Aliongeza kuwa "maisha yake yamebadilika na kuwa mabaya sana " na kwamba "hatakuwa mtu wa kawaida tena ".

Apple "ilimsukuma " "kuwa na hisia za maoenzi ya jinsia moja kupitia ushawishi wake", alidai.

"Mabadiliko ya kijinsia yamenisababishia mabadiliko makubwa ya kimaadili na madhara ya kiakili."

Sapizhat Gusniev anasema kampuni ya Apple "inawajibika na programu zake " licha ya madai ya mabadiliko yanayofanywa na app nyingine kwenye simu hizo.

Mnamo 2013, Urusi ilianzisha sheria dhidi ya " uhamasishaji wa mapenzi ya jinsia moja", ambayo inapiga marufuku rasmi "kueneza mitindo ya maisha ambayo ni kinyume na maisha ya kawaida kwa watoto na vijana wadogo " .

Mahakama itamsikiliza mlalamikaji tarehe 17 Octoba, kwa mujibu wa taarifa yake kwenye wavuti.

Apple bado haijatoa kauli yoyote kuhusiana na shutuma hizo dhidi yake.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?