Je IMF inarudisha msaada kwa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo?

Serikali ya Kinshasa inasema shirika la fedha la kimataifa (IMF) linafikiria kuidhinisha upya ushirikiano wa kifedha na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika miezi sita ijayo, Reuters linaripoti.

IMF lilisitisha msaada wa kifedha wa serikali ya Congo miaka takriban miaka 7 iliyopita chini ya utawala wa rais Joseph Kabila baada ya serikali hiyo kushindwa kutoa taarifa za kutosha kuhusu mauzo ya madini nchini kwa kampuni iliyoko ng'ambo.

Katika taarifa kufuatia kikao cha baraza la mawaziri, serikali imesema: " IMF litakagua katika muda wa miezi misita mpango wa muda mfupi na serikali." taarifa hiyo haikutoa maelezo zaidi, kwa mujibu wa vyombo ya habari.

IMF linafikiria ushirikiano mpya wa kifedha na amhuri ya Kidmokrasi ya Congo kufuatia majadiliano mapya kati ya pande hizo mbili, Bloomberg imemnukuu waziri mkuu wa Congo Sylvestre Ilunga.

Katika ripoti yake 'Article IV consultation' mapema wiki hii , IMF limeeleza kuwa wakurugenzi wake wamekaribisha majadiliano mpaya ya serikali ya Kinshasa na IMF, na kusisistiza kuwa mageuzi ya amani ya kisiasa nchini humo yanatoa fursa kuidhinisha mageuzi yatakayoweza kuimarisha mifumo ya fedha za umma, kushinikiza ukuwaji wa sekta na kukabiliana na ufisadi naumaskini nchini.

Kadhalika shirika hilo limeeleza kuwa limetambua kwamba 'Congo inahitaji usaidizi wa jamii ya kimataifa na usaidizi wa kujenga uwezo'.

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebarikiwa kuwa na madini mengi pamoja na maliasili lakini zimeathiriwa na vita vinavyosababishwa na vikundi vya waasi ,rushwa, machafuko ya kisiasa na hivi sasa janga la Ebola.

Congo ni mchimbaji wa madini ya cobalt, shaba, dhahabu, tin na almasi lakini taifa hilo linasalia kuwa mojawapo ya mataifa yanayoshuhudia maendeleo duni duniani




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?