Manchester City: Pep Guardiola anaamini timu yake inaweza kuifikia Liverpool

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema "pengo ni kubwa" lakini bado anaamini timu yake inaweza kuifikia Liverpool katika kinyang'anyiro cha kuwania taji la ligi kuu England.

Pigo la Wolves 2-0 dhidi ya City ina maana sasa klabu hiyo ipo nyuma kwa pointi nane nyuma ya Liverpool.

Ni tofauti kubwa iliyowahi kuwepo baada ya mechi nane katika ligi kuu ya England - Timu ya awali iliowahi kuwa katika nafasi hiyo ni Chelsea mnamo 2014, ilioishia kushinda taji.

Ninawafahamu hawa jamaa," anasema Guardiola. "Bado wanajikakamua na bado wanaweza kushinda."

Kushindwa huko kuna maanisha kuwa City inakabiliwa na mwanzo mbaya kuwa kushuhudiwa tangu kampeni ya 2013-14 chini yake Manuel Pellegrini, wakati waliposogea na kushinda taji.

Liverpool ilizuia rekodi yake ya 100% Jumamosi kutokana na jeraha alilopata James Milner lililompatia penalti dhidi ya Leicester.

"Pengo ni kubwa, hilo najua," anasema Guardiola. "Kwa wakati mwingi, [Liverpool] haikushuka kwa pointi. Ni vyema kutofikiria timu moja iko pointi nane mbele. Ni oktoba tu hii. bado kuna mechi nyingi."

Pengo kubwa iliokuwa nayo City ambalo ilibidi kuliziba dhidi ya Liverpool msimu uliopita ilikuwa ni la pointi 10, licha ya kwamba hilo lilikuwa ni baad aya mechi 19 na ikisalia na mechi moja na timu hizo zililazimika kucheza mara moja . Timu hizo mbili zinakutana kw amara ya kwanza Anfield Novemba 10.

City inapania kuwa timu ya kwanza kushinda mataji matatu ya ligi tangu Manchester United kati ya 2007-09. Wakati wa mwisho walikuwa timu ya kwanza kulishikilia taji hilo tangu wakati huo. Chelsea ndio timu nyingine iliowahi kushinda mataji kwa mtawalia katika enzi ya Premier League.

Timu nyingi zilizoshinda siku za nyuma, mwaka uliofuata hazikushinda," anasema Guardiola.

City imeshindwa kushinda mechi mbili za ufunguzi nyumbani kwa mara ya kwanza tangu 2014. Tayari timu hiyo imeshukwa kwa pointi tano nyumbani pointimbili zaidi ya msimu mzima uliopita.

Mwaka uliotangulia, walipoweka rekodi ka kufika pointi 100 walishuka kwa pointi 7 uwanjani Etihad katika kampeni nzima.

Kabla ya mechi dhid ya Wolves, City ilikuwa ndio timu kati ya 'sita kubwa' 'ambayo Wolves ilishindwa kuifunga tagu kuanza kwa msimu, ikiwa imezifunga nyingine kwenye ligi na kuwahi kuiondoa Liverpool kutoka kwenye kombe la FA.

"Ilikuwa ni siku mbaya," anasema Guardiola. " Nilihisi siku ya leo itakuwa ndio siku ambayo hatutakuwa na mapato. Tumekabiliana na timu nyingi zenye ulinzi mkali na kwa namna moja au nyingine tumepata njia ya kulishughulikia hilo, lakini leo tulikuwa na shida."



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?