Mgogoro wa Syria: Je Muungano mpya wa Urusi, Uturuki na Syria unaiweka wapi Marekani?

Rais wa Urusi Vladimir Putin alikutana na mwenzake wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan siku ya Jumanne ili kushinikiza jukumu la Moscow kama mdhamini aliyesalia wa uthabiti wa eneo la kaskazini mwa Syria.

Mataifa yote mawili yataanza doria za pamoja ili kusaidia kuweka mpaka mpya unaojulikana kama eneo la usalama.

Kwa upande mwingine magari ya vikosi vya jeshi la Marekani ambayo yalikuwa yakiondoka nchini Syria yanarushiwa mboga na uchafu yalipokuwa yakiondoka na kuwaacha washirika wake wa Kikurdi.

Uvamizi wa Uturuki nchini Syria na kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kuna athari kubwa kwa Syria na eneo hilo kwa jumla.

Baadhi ya athari hizo ni za moja kwa moja huku nyengine zikitarajiwa katika siku za baadaye.

Je ni muungano utakaoibuka mshindi?

Huo ni ushindi kwa Waturuki, kwa Urusi na serikali ya Syria.

Kwanza Uturuki imepata kile ilichokuwa ikitaka: Inaendelea kuwaweka wanajeshi wake pamoja na washirika wake katika eneo hilo ambalo tayari inalidhibiti.

Urusi na Syria zinaonekana kukubaliana kusimamia kuondoka kwa vikosi vya Kikurdi kutoka katika eneo kubwa ambalo linavuka mpaka wa Uturuki na kuingia nchini humo.

Taifa hilo limekua likiisaidia Syria kijeshi kwa muda mrefu likiwa ndio taifa la pekee linaloweza kufanya majadiliano kama hayo.

Urusi imerudi mashariki ya kati na licha ya uovu wa mashambulizi yake ya angani nchini Syria imeonesha kwamba mbali na Marekani ni mshirika muaminifu ambaye anaweza kuzaa matunda.

Kwa upande wa serikali ya Syria pia kuna habari njema.

Rais Bashar al-Assad anaendeleza udhibiti wake hadi kaskazini , ijapokuwa atalazimika kukubali uwepo wa Uturuki katika eneo la Syria.

Hii ni hatua nyengine ya kuhakikisha ushindi kwa utawala wa Syria, kitu ambacho mwanzo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe wachanganuzi wengi walidhania kwamba haiwezekani.

Uturuki, Urusi na Syria kwa sasa zinakubaliana. Lakini je makubaliano yao yatadumu kwa muda gani?.

Je Wakurdi watasema nini? Wao ndio wanaokabiliwa na wakati mgumu, lakini je watakuwa waatifu kwa muungano huo wa Uturuki na Urusi?.

Je watachukua hatua gani mbadala iwapo ipo?.

Kuna hofu kuhusu mabomu 50 ya Kinyuklia ambayo Marekani inahifadhi nchini Uturuki karibu na mpaka na Syria.

Kuanguka kidiplomasia

Iwapo Wakurdi ndio watakaopoteza moja kwa moja , Marekani itakuwa imepoteza zaidi kidiplomasia.

Rais Donald Trump huenda alifanya uamuzi mzuri kumaliza vita vya kigeni, kwa ufupi ni wazo linaloungwa mkono na wengi nchini Marekani.

Lakini kuna njia na uwezo wa kutekeleza jambo kama hilo.

Kuondoka kwa vikosi vya Marekani ambako kunawaacha washirika wake katika hatari, kunatuma ishara mbaya wakati ambapo ufahari wa Marekani na uaminifu wake umezua maswali mengi.

Jinsi Marekani ilivyoangazia 'mashambulio' ya Iran dhidi ya hifadhi za mafuta za Saudia pia ni swala lililozua maswali mengi.

Shambulio hilo lililoonesha udhoofu wa idara ya ulinzi ya Saudia lilifanyika bila jibu lolote kutoka kwa Marekani.

Usiwe mjinga! Ni barua ya rais Trump iliomkasirisha rais Erdogan kabla ya Uturuki kuanza mashambulio nchini Syria.

Washington inaonekana ilifurahia kwamba Saudia ililivalia njuga swala hilo huku ndege za kivita za Marekani zikipelekwa nchini humo ili kuweka ulinzi hatua iliochelewa na hivyobasi kushindwa kuimarisha imani ya Saudia iliovunjwa.
Kwa wengi katika Ghuba na Israeli, rais Trump anazungumza kwa majigambo lakini haaminiki.

Haya ni mambo ambayo yamekuwa katika vinywa vya wachanganuzi wengi kwamba uamuzi wa rais huyo kuhusu maswala ya kigeni unaonekana kukosa mkakati.

Na maamuzi yake ni kinyume na jinsi rais Putin anavyofuatilia swala hilo.

Rais huyo wa Urusi alichukua fursa ya kuisaidia serikali ya rais Assad na hivyobasi kuifanya Urusi kuonekana kama mshirika muhimu katika diplomasia ya eneo hilo na kumvutia mwanachama muhimu wa shirika la Nato kama Uturuki katika mduara wake .

Hajafurahia huruma ya Marekani kwa Wakurdi waliopo nchini Syria kwa muda mrefu.

Hatahivyo licha ya kwamba Urusi inafaidika kutokana na kufeli kwa Marekani hakumaanishi kwamba inabadilisha fursa yake ya kimkakati.

Ukweli ni kwamba uwezo wa Urusi wa kushirikiana na Uturuki unaongeza joto zaidi katika swala hilo.

Wanachama wengi wa Nato wameshindwa kuelezea ufahamu wao kuhusu hofu ya kiusalama ya Uturuki.

Lakini ni wazi kwamba Uturuki kwa sasa ipo katika njia ambayo inaiondosha katika muungano wa Nato na kwa jumla kutoka kwa mataifa ya magharibi.

Hatahivyo hii ni Uturuki ambayo mapema mwaka huu ilinunua mfumo wa kujilinda na makombora kutoka kwa Urusi , uamuzi ambao haukutarajiwa na wawakilishi wa Nato.

Iwapo mkakati wa utawala wa rais Trump utaendelea kuyumbayumba, basi athari za muda mrefu za matukio hayo huenda zikazingatiwa na kufanya kazi katika mweleko unaokinzana.

Katika eneo la Ghuba, jibu la Saudia na washirika wake linaonekana kuwa la tahadhari katika kukabiliana na Iran.

Je wapiganaji wa Islamic State watapelekwa wapi?

Swali jingine kuu ni athari gani ambazo hatua hii ya Urusi, Syria na Uturuki itasababisha katika eneo la kaskaini mashariki mwa Syria dhidi ya kundi la wapiganaji wa Islamic State.

Ukweli ni kwamba hofu kuu ya mataifa ya magharibi ni kwamba kuna uwezekano wa ghasia za IS huku wapiganaji hao wakitoroka kutoka katika kambi ama vituo ambavyo walikuwa wakizuiliwa.

Je maeneo haya yataendelea kuwa salama?

Na je itakuwaje iwapo wanajeshi wa Uturuki, Syria na Urusi watakabiliwa na ghasia hizo, je watazikabili?









Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Watalii wa Ufaransa kukabiliana na hukumu ya wizi wa mchanga