Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 23.10.2019: Sancho, Alena, Mandzukic, Ibrahimovic, Morelos, Diaz

Mchezaji wa zamani wa Liverpool wa safu ya kati Dietmar Hamann anasema kuwa amepata fununu kwamba Reds "wanahamu sana" ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19. 


Mancheter United huenda ikaongeza juhudi ya kumsajili Mario Mandzukic, 30, baada ya mshambuliaji wa Juventus na Croatia kupunguza masharti ya marupu rupu yake. 

Real Madrid imemwambia kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City Brahim Diaz, 20, kwamba inataka kumuuza kama sehemu ya kuondokeana nae kabisa. 

Mchezaji wa safu ya kati ya Real Isco, 27, amekubali kuwa mmoja wa wachezaji watakaoondoka klabu hiyo mwezi January mwakani. 

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Paris St-Germain na Juventus, Zlatan Ibrahimovic,38, anataka kurejea katika ligi kuu ya Italia, Serie A.

Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Uswidi katika klabu ya LA Galaxy unakamilika mwisho wa mwaka huu. 

Barcelona imepinga madai kuwa imeilipa Atletico Madrid euro milioni 15 kumaliza mzozo kati yake na klabu hiyo kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28. 

Juventus na Atletico Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia beki wa West Brom Nathan Ferguson, 19. 

Meneja wa chuo cha mafunzo ya soka ya Manchester United Nicky Butt anasema klabu hiyo inawachezaji wengi ambao wanaweza kufuata nyayo za mshambuliaji Marcus Rashford na kuleta mabadiliko katika kikosi cha kwanza. 

Crystal Palace itamenyana na Aston Villa katika juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos, 23, kutoka Rangers mwezi Januari. 




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?