Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 25.10.2019:Rodwell, Muller, Mourinho, Chilwell, Maddison, Sidibe

Kiungo wa kati wa Manchester City Jack Roderll,28 , yuko kwenye mazungumzo na Roma kuhusu kuhamia Serie A 

Manchester United wanamtolea macho mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Thomas Muller, 30. 

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc amekana uvumi kuwa kocha wa zamani wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho kuwa ataelekea kwenye klabu hiyo ya Ujerumani. 

Manchester United haitarajii kuwasajili Ben Chilwell wa Leicester au James Maddison, 22, mwezi Januari.

Monaco haiwezi kumuita tena mlinzi wa timu ya Ufaransa Djibril Sidibe, 27, kutoka Everton anakochezea kwa mkopo, kutokana na tetesi kuwa mfaransa huyo anahusishwa na kuelekea AC milan.

Paul Scholes anaamini klabu yake ya zamani Manchester United ijaribu kumsajili mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil,31, ili kutatua tatizo la safu ya ushambuliaji 

Leicester wanahusishwa na taarifa kuwa wana mpango wa kumsajili kiungo Kerem Baykus,19. 

Mkurugenzi wa Wolves sporting Kevin Thelwell anasema uhamisho wa mkopo haumfai kiungo wa kati Gibbs-White, akisisitiza kuwa mchezaji huyo, 19 ''hajashindwa'' 

Crystal Palace wamepata pauni milioni 22.5 baada ya kumuuza mchezaji wa nafasi ya ulinzi Aaro Wan-Bissaka,21, kwenda Manchester United.

Manchester City nusura wamkose Pep Guardiola kutokana na kukosekana kwa mazingira mazuri ya klabu hiyo.

Kiungo wa kati Ronald de Boer,49, karibu ajiunge na Manchester United mwaka 2000 lakini alishauriwa kutofanya hivyo na aliyekuwa kocha wa wakati huo Louis Van Gaal, ambaye alienda kuwa meneja wa United mwaka 2014.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?