Je, unajua namna ya kumpima nyangumi bila ya mizani?

Unaweza kumpima vita uzito mnyama mkubwa duniani?

Kufikia sasa hilo limewezekana tu pale wanaposombwa na maji hadi katika fukwa za bahari.

Wanasayansi sasa wamelitatua hilo kwa usaidizi wa picha za kieneo zilizopigwa kwa ndege zisizokuwa na rubani.

Wamefanikiwa kuhesabia uzito wa mwili wa nyangumi wa wanaopatikana kusini mwa bahari za Atlantic na Pasifiki.

Tayari mfumo huo unatumika kukagua uhai wa watoto wa nyangumi hao na ina manufaa mengi katika uhifadhi wao.

Uzito wa mwili ni suala muhimu katika ufanisi wa nyangumi kama kundi, kubaini mahitaji ya nguvu, vyakula na viwango vya ukuwaji.

Baadhi ya tunayoyafahamu kuhusu ukubwa wa miili ya nyangumi unatokana na mifano ya wanyama wanaosombwana maji hadi katika fukwe za bahari.

"Ni vigumu kumpima nyangumi kwenya mizani - maana ni lazima umuue ili kuweza kulifanya hilo. Na ndilo jambo linalojaribu kuzuiliwa hapa," asema mtafiti Fredrik Christiansen kutoka taasisi ya Aarhus Institute of Advanced Studies nchini Denmark.

Watafiti waliwachunguza nyangumi hao, wanaokusanyika kwa idadi kubwa kutoka pwani ya Argentina.

Walifanya nini?

Waliipeperusha ndege isiyokuwana rubani juu ya nyangumi waliokuwa wakiogelea majini, na kunasa picha wakati nyangumi wakubwa na wadonga walipokuja juu ya maji kupumua, ikiwemo migongo yao, ubavuni mwao na wakati walipojizungusha majini.

Ni kutokana na picha hizo walifanikiwa kupata urefu, upana wa nyangumi 86.

Waligundua wanaweza kupata uwakilishi mzuri wa umbo la miili ya nyangumi hao ambalo walilimithilisha na yaliofahamika kuhusu urefuna uzito wa nyangumi.

Walifanikiwa kisha kugeuza umbo la mwili na ukubwa kuwa kipimo cha uzito.

"Uwezo wa kutambua uzito wa mwili wa nyangumi walio hai unatoa fursa kwetu kuwaangalia wanyama na kutazama namna wanavyobadilika na namna wanavyokuwa," amesema Prof Christiansen.

Utafiti wa kutumia ndege hizo zisizokuwana rubani unaweza kusaidia katika uhifadhi na uangalizi wa afya ya jamii tofuati za nyangumi baharini.

Huenda mtazamo huo ukatumiwa pia kukadiria idadi ya wanyama wengine wa baharini .

Utafiti huo umefanyika kwa ushirikiano na shirika la uangalizi wa afya ya nyangumi Southern Right Whale Health Monitoring Programme nchini Argentina na taasisi ya Woods Hole Oceanographic Institution nchini Marekani.

Na umechapishwa katika jarida la British Ecological Society - Methods in Ecology and Evolution (MEE).




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?