Virusi vya Corona: Waandamanaji wataka marufuku ya kutokutoka nje iondoshwe Marekani kufungua uchumi

Waandamanaji nchini Marekani wameingia mitaani katika majimbo kadhaa wakishinikiza magavana kufungua uchumi wa majimbo yao kwa kuondosha amri ya kutokutoka nje ama 'lockdown'.
Marufuku hiyo ya kutokutoka nje imewekwa katika majombo yote ya Marekani ili kudhibiti kusambaa kwa janga la virusi vya corona, hali iliyotikisa uchumi wa taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi duniani.
Maaandamano yameripotiwa jana Jumapili katika majimbo ya Arizona, Colorado, Montana na Washington, huku mwendelezo wa maandamano hayo ukitarajiwa leo Jumatatu.
Hasira juu ya marufuku hizo imeongezeka nchini humo huku waandamanaji wakitaka masharti yalegezwe licha ya hatari ambayo ingalipo ya maambukizi ya virusi vya corona.
Rais wa Marekani Donald Trump ameoesha dalili za kukubaliana na maandamano hayo.
Kwa sasa, Marekani ndiyo kitovu cha janga la ugonjwa wa virusi vya corona (Covid-19), kukiwa na wagonjwa zaidi ya 735,000 na vifo zaidi ya 40,000.
Hata hivyo kuna dalili kuwa maambukizi yanafikia kileleni nchini humo na kasi ya maambukizi kuanza kushuka katika baadhi ya majimbo.
Magavana katika majimbo mbalimbali wameanza majadiliano ya kufungua uchumi baada ya kushuhudiwa kupungua kwa maambukizi, lakini maeneo mengine bado yangali kwenye marufuku kali.
Gavana wa jimbo la California Gavin Newsom alikuwa wa kwanza kutoa amri ya watu kusalia nyumbani katika jimbo lenye watu wengi zaidi nchini humo toka Machi 19.
Majimbo jirani ya Washington na Oregon yakafuatia siku chache baadae na kufanya jumla ya watu milioni 11.5 wa majimbo hayo mawili kusalia ndani toka Machi 23.
Gavana wa New York Andrew Cuomo ametangaza wiki hii ametangaza kuongeza muda wa marufuku hiyo jimboni mwake mpaka kufikia Mei 15.
Akizungumza jana Jumapili Cuomo aliwataka wakazi wa jimbo hilo ambalo imeathirika zaidi kwa Marekani kujitenga na shauku ya jimbo lao kufunguliwa tena
Bado tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunakidhibiti kirusi hiki," amesema Cuomo. "Wakati ambao wote tukiwa na shauku na tukijiandaa kurejea katika maisha ya kawaida."
"Kwa sasa tupo tu mapumziko (baada ya kuisha kipindi cha kwanza) katika janga hili."
RaisTrump, ameonekana kuridhia maandamano hayo dhidi ya hatua kali za marufuku, akisema siku ya Ijumaa kuwa hatua zinazotekelezwa katika majimbo ya Minnesota, Michigan na Virginia "ni ngumu sana".
Hatua hizo hata hivyo zinahitajika ili kuzuia kusambaa kwa virusi.

'Ni jambo la hatari'

Gavana wa jimbo la Washington Jay Inslee ameita uungaji mkono wa rais Trump kwa waandamanaji hao kuwa ni kambo la "hatari", sawa na kuchochea "kutotekelezwa" kwa sheria za majimbo.
"Kuwa na rais wa Marekani ambaye anachochea watu kuvunja sheria, sikumbuki ni lini katika historia ya Marekani kuwa na kitu kama hicho," Gavana Inslee ameiambia runinga ya ABC.
Spika wa Bunge la Kongresi Nancy Pelosi amemtuhumu Trump kwa kuridhia maandamano hayo.
"Raisi anaridhia maandamano kama njia ya kufanya watu wasahau kuwa hakuwa na umakini katika vipimo, matibabu, kufuatilia waliokutana na wagonjwa na karantii kwa usahihi kwa usahihi na karantini," Pelosi pia ameiambia runinga ya ABC.
Maandamano pia yamefanyika katika majimbo ya Denver, Colorado, Phoenix na Arizona.
Jimboni Denver, waandamanaji waliiandamana mpaka katika jengo la baraza la kutunga sheria la jimbo kupinga amri za kujitenga. Magari kadhaa yalizunguka jengo hilo huku waandamanaji zaidi ya 200 wakisimama pembeni wakipeperusha bendera.
Jumamosi, waandamanaji walitengeza msongamano wa magari katika mitaa ya jiji la Annapolis, jimboni Maryland, wakipiga honi kupinga amri ya marufuku ya kutoka nje.
Zaidi ya magari 200 pia yaliendeshwa mpaka nje ya makazi ya gavana wa jimbo la Indiana governor, huku 200 pia yakikusanywa katika jiji la Austin, jimboni Texas.
Majimbo ya Utah, Washington na New York pia yalishuhudia rabsha pia Jumamosi.
Maandamano zaidi yanatarajiwa leo.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?