Virusi vya Corona: Barakoa ipi ni sahihi kwa matumizi?

Barokoa,glovu na vifaa vingine vya kujikinga vinavyoweza kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona iwapo vitatumika sahihi.
Shirika la afya duniani-WHO inasema ni aina mbili tu za watu wanafaa kuvaa barakoa , nao ni :
  • Wanaoumwa na wanaoonyesha dalili
  • Mhudumu wa watu wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Corona
Kwanini sio kila mtu anapaswa kuvaa?
Barakoa za upasuaji hazijapendekezwa kwa matumizi ya umma kwa sababu::
  • Vinaweza kuchafuliwa na kikohozi vya watu wengine au unapopiga chafya au unapoivaa na kuivua
Virusi vya corona vinaweza kusambazwa kwa matone ambayo yanaweza kusambaa hewani, pale ambapo wale walioambukizwa wakiongea, wakikohoa au kupiga chafya.
Virusi hizo vinaweza kuingia mwilini kupitia macho na mdomo au au baada ya kugusa vitu vilivyopata maambukizi.
Lakini kama hawa watu wakivaa barakoa haya matone yanaweza kupunguzwa .
Haishauriwi kutumia barakoa iliyotengenezwa nyumbani kwa sababu hakuna uhakika kuwa itatoa kinga ya kutosha au la.
Hata kama barakoa hizo za nyumbani zikitumika kwa usahihi, lakini kitambaa hakijathibitishwa kuwa na ubora wa kinga hivyo ni vinaweza kuwa hatari kwa maambukizi, anasema hivyo mshauri kutoka ulaya.
Mara nyingi kitambaa hicho kinatumika zaidi ya mara moja.
Katika hospitali barakoa za aina tofauti zinatoa ulinzi wa viwango tofauti.
Inayotoa ulinzi bora zaidi ni FFP3 au N95 au FFP2 ina kifaa cha kupumilia ambacho uchuja hewa mtu anayovuta
Wataalam hawashauri umma kutumiwa hizi ni kwa ajili ya wahudumu wa afya ambao wapo karibu zaidi na wagonjwa wa corona na wapo katika hatari kubwa ya kukumbana na majimaji ya njia ya hewa kutoka kwa waathirika.

Nini kingine tunaweza kutumia kujikinga na virusi vya Corona?

Glovu pamoja na mavazi mengine ya kujilinda yanashauriwa kutumiwa na wahudumu wa afya walio kwenye maeneo wanayoweza pata virusi vya Corona
Tena, wafanyakazi walio katika hatari kubwa zaidi wanashauriwa kuvaa barakoa zenye ulinzi mkubwa zaidi na sio za vitambaa vya kawaida, glovu, barakoa na miwani ya kujikinga.
Umma haushauriwi kutumia gloves au vifaa zaidi vya kujikinga
Kujilinda dhidi ya virusi vya Corona unashauriwa yafuatayo:
  • Nawa mikono kwa maji na sabuni mara Kwa mara, angalau kwa sekunde 20 na mara tu baada ya kurudi nyumbani
  • Tumia sanitizer kama hakuna maji na sabuni
  • Ziba mdomo wako kwa tishu au kitambaa na sio mikono yako ukiwa unapiga chafya ,weka tissu uliotumia katika pipa la taka na unawe mikono yako
  • Usishike Macho,pia au mdomo kama mikono yako michafu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?