Coronavirus: Makanisa mashuhuri nchini Nigeria yakosa waumini

Makanisa makubwa makubwa nchini Nigeria sasa hayana watu na milango imefungwa huku kila mmoja akilazimika kufuata marufuku iliyowekwa na serikali ya kutokusanyika ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.
Lakini hilo kufanyika, sio tu vitisho vimetolewa, lakini maafisa wametumia nguvu na watu kukamatwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Kwa baadhi ya visa maafisa wamelazimika kuchukua hatua moja kwa moja.
"Naomba kutumia maneno [Mtume] Mordechai: 'Kwa wakati kama huu tunachukua hatua ambazo ni sahihi, "Amesema kiongozi wa vikosi vya usalama mjini Abuja wakati anamkamata kasisi mmoja mbele ya waumini wake.
Kasisi huyo aliyekuwa amevalia nadhifu alionekana kuwa miongoni mwa watu mashuhuri ambao kwasasa wanaongoza waumini wengi katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.
Makasisi siku hizi wamebadilisha Ukiristo nchini Nigeria kwa mahubiri yao, utabiri na ahadi zao za maiujiza.

Nadharia za kihasidi

Mmoja wa wahubiri ambao ni mashuhuri ni TB Joshua, ambaye wiki iliyopita alidai kwamba ameoteshwa na Mungu na kutabiri kuwa janga la Corona litamalizika kufikia Machi 27, siku kadhaa kabla ya amri ya kukaa nyumbani kutangazwa katika mji wa Lagos, Ogun na mji mkuu wa Abuja.
Kufikia mwisho wa mwezi huu, ama tunataka au la, haijalishi dawa ambayo watakuwa wameivumbua ugonjwa huu utatoweka kama ulivyoingia," alisema hivyo huku mkusanyiko wake ukimpigia makofi.
Machi 27 ilipopita, mhubiri huyo ambaye huubiri katika televisheni alijipata akikejeliwa kwa utabiri wake wa uwongo.
Lakini akajitetea na kwa mara nyengine tena akiwa mbele ya umati uliokuwa umekuja kuabudu, alisema: "Nilicho maanisha ni kwamba ugonjwa huu utamalizikia pale ulipoanza katika mji wa Wuhan ambako tayari umedhibitiwa."
Wahubiri wengine wameshtumiwa kwa kupinga uwepo wa virusi hivyo mbele ya mamlaka na kusambaza taarifa za uwongo jambo ambalo ni kikwazo katika juhudi za kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.
Utata mkubwa umesababishwa na mhubiri Chris Oyakhilome, ambaye katika video iliyosambaa mitandaoni, alihusisha virusi vya corona na teknolojia ya mawasiliano ya 5G na kudai kwamba ilikuwa sehemu ya njama ya kuunda amri mpya duniani.
Maoni kama hayo yameshtumiwa vikali na wanasayansi ambao wanasema kuwa wazo la kuhusisha Covid-19 na teknolojia ya mtandao ya 5G ni upuuzi mtupu na kibaolojia ni jambo lisilowezekana kabisa.

Maombi kupitia mitandao ya kijamii

Kwa baadhi ya waumini wa Kikirsto, hasa wale ambao ni wa madhehebu ya makanisa ya Anglican na katoliki, juhudi zaidi zinahitajika kufanywa kupunguza ushawishi wa wahubiri ambao ni maarufu na watumia vibaya wafuasi wao.
Wale ambao wanasema wana nguvu za kufanya miujiza, wenye mafuta ya upako na mambo kama hayo, huu ndio wakati wa kuthibitisha ambayo wamekuwa wakiambia wafuasi wao," amesema Bi. Blessing Ugonna kutoka Lagos.
Lakini makanisa mengi, ambayo yamekuwa biashara yenye kuleta mamilioni ya pesa yamekubali mabadiliko yaliyojitokeza kwasababu ya Corona.
Wanafanya maombi yao mitandaoni, huku familia zingine zikijaribu kutengeneza mazingira sawa na kanisani kwa kuva vizuri kila Jumapili kiasi hata cha kuokota sadaka kutoka kwa baadhi ya wanafamilia ili kuitoa kanisani.
Makanisa pia yanatoa ufadhili kwa serikali na katika hatua ambayo kuna uwezekano mkubwa wakaendeleza umaarufu wao.
Mhubiri Enoch Adeboye - mkuu wa kanisa la Redeemed Christian Church of God ambalo lina matawi yake katika maeneo mengi ya miji ambayo ina waumini wengi wa Kikirsto pamoja na kusini mwa Nigeria - limechangia glovu 200,000, vitakasa mikono (hand sanitisers) 8,000, barakoa 8,000 kwa serikali ya mji wa Lagos.
Na kanisa la Mountain of Holy Ghost Intervention - linaloongozwa na Chukwuemeka Odumeje ambaye kuna wakati alisambaa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kuwapa watu chakula walio katika hatari ya kufa kwa njaa katika kipindi cha wiki mbili cha amri ya kusalia ndani.

Miji isiyokuwa na waumini licha ya kuwa ni wiki takatifu

Aidha, waumini wengi wa Kikiristo bado wana hamu kubwa ya kwenda kanisani na hasa Jumapili iliyopita kwa sababu ilikuwa jumapili ya Matawi.
Kawaida, mitaa ya Lagos huwa na watu wengi wanaotembea huku wakiwa wameshika matawi wakiigiza kuwasili kwa Yesu kabla ya kusulubiwa.
Mitaa haikuwa na watu kabisa mwaka huu, na kuna uwezekano mkubwa hali ikaendelea kuwa hivyo kipindi cha msimu sikukuu ya pasaka.
Lakini kuna kundi la watu wanne - wanawake 3 na mwanaume 1 wawaliokutana na mwandishi wa Newsday Swahili wakirejea kutoka kwa misa ndogo iliyofanyika katika nyumba ya mmoja wao
Walipoulizwa kwanini wamepuuza ushauri wa kuomba kila mmoja peke yake nyumbani kwake, mmoja wao alisema: "Hata bibilia inasema pale 2 au 3 wanapokusanyika, Mungu yuko pamoja nao. Bibilia haikusema mtu mmoja."
'Mashujaa wa maombi'
Kisha mwandishi wa BBC akaenda makao makuu ya kanisa la Mountain of Fire and Miracles Ministries, ambalo linafahamika kwa maombi katika jimbo la Ogun.
Walinzi walimuarifu kwamba hakuna huduma inayoendelea kwa sasa.
"Hakuna hata huduma ya mtandaoni?" aliuliza.
"Hakuna hata huduma ya mtandaoni," mmoja wao, aliyekuwa amevaa fulana ya rangi ya chungwa, alimjibu.
"Kwahiyo wanaendeleza vipi Imani zao?" Aliuliza.
Mmoja wa walinzi akaingiza mkono ndani ya mkoba wake na kutoa kijitabu kidogo na kumkabidhi.
"Hicho ndicho wanachosema kipindi hiki cha amri ya kukaa ndani," alisema, kabla ya mlinzi kufunga mlango.
Kijitabu hicho kimepewa jina la ''Thirty Days Prayer Retreat'' kwa kiingereza - kikinukuu baadhi ya aya katika bibilia.
Haitakuwa jambo la kustaajabisha kuona wale wanaojiita mashijaa wa maombi wakimaliza kusoma kijitabu hicho ndani ya siku 14 za mari ya kutotoka nje, badala ya mwezi.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?