Virusi vya corona: Kutokaribiana na kujitenga ni nini haswa?

Watu wanastahili kusalia nyumbani kusaidia kuzuia kusambaa kwa coronavirus serikali imesema.
Sheria zilizowekwa kukabiliana na ugonjwa huu zinasema kwamba watu wanastahili kutoka iwapo tu kutakuwa na haja ya kufanya hivyo na kama kuna sababu ya msingi. Hiyo ni pamoja na:
  • Kufanya mazoezi peke yako au ukiwa pamoja na familia yako.
  • Kufanya manunuzi ya bidhaa za msingi
  • Kama unahitaji kupata matibabu, ama pengine unasaidia mtu mwenye mahitaji maalum.
  • Kama unakwenda au unatoka kazini lakini ikiwa tu huwezi kufanyakazi kutoka nyumbani
Je sheria zinazostahili kufuatwa ni zipi wakati wa kufanya mazoezi?
Ikiwa ni lazima utoke nje, huna budi zaidi ya kukaa umbali wa mita 2 kutoka alipo mwengine mbali na watu wa familia yako. Hii ndio kwa kiingereza inafahamika kama 'social distancing'.
  • Mwongozo wa serikali unasisitiza watu kusalia majumbani, kutumia maeneo ya wazi yaliokaribu na nyumba zao na kutosafiri
  • Mwongozo wa polisi unasema kwamba watu hawastahili kuwekewa vikwazo vya kusafiri katika umbali ambao utakuwa ni kama kufanya mazoezi - ingawa hilo halijafafanuliwa.
  • Watu watafanya mazoezi mara moja kwa siku, ingawa Uingereza, Scotland na Kaskazini ya Ireland hakuna marufuku ya watu kutofanya mazoezi zaidi ya mara moja kwa siku. Wales, ambayo inajitungia sheria zake yenyewe, kwasasa ni marufuku kufanya mazoezi zaidi ya mara moja kwa siku kwasasa na hilo linaweza hata kuchukuliwa kama kosa la uhalifu
  • Unaweza kufanya mazoezi peke yako ama ukiwa pamoja na wanafamilia wengine
  • Kukusanyika kwa watu zaidi ya wawili katika maeneo ya bustani na ya wazi kumepigwa marufuku
  • Pia mbwa wanaweza kutembezwa kama sehemu ya kufanya mazoezi
Suala la unaweza kufanya mazoezi kwa muda gani bado halijawekwa wazi. Waziri husika Michael Gove amesema: "Kwangu nataka kufikiria kwamba wengi wangefanya mazoezi ya viungo kwa saa moja, kukimbia kwa dakika 30 ama hata ukatumia baiskeli yako kwa muda huo, kulingana na uwezo wa mtu wa kufanya mazoezi, inakubalika."
Baada ya watu kuonekana wakiota jua wakati wa joto. Waziri wa afya Matt Hancock amesema hilo lilikuwa linakinzana na sheria ya kutosongeleana.
Aidha, maafisa wa polisi wamepewa nguvu ya kusaidia katika makabiliano dhidi ya virusi vya corona kwa kuhakikisha hatua za kutosongeleana zinatimizwa.

Kwanini ni lazima kutokaribiana?

Kutosongeleana ni jambo la msingi kwasababu kusambaa kwa coronavirus kunatokea ikiwa mtu aliyeambukizwa atakohoa kidogo na kurusha chembechembe zenye virusi kwenye hewa.
Hewa hiyo inaweza kuvutwa ndani ama inaweza kusababisha maambukizi iwapo utagusa sehemu ambazo chembechembe hizo zimefika kisha ukagusa uso kwa mikono yako ambayo haijaoshwa.

Lakini kujitenga ni nini?

Iwapo utaonesha dalili za coronavirus - kama vile kuwa na kikohozi kikavu na nyuzi joto ya juu - lazima uchukue tahadhari zaidi.
Unastaili kusalia nyumbani na ikiwezekana, usitoke isipokuwa tu kufanya mazoezi mara moja kwa siku (na kuhakikisha uko umbali wa mita 2 kando na wengine).
Hili ndio linalofahamika kama kujitenga au self-isolation kwa kiingereza.
Ikiwezekana, usiende nje hata kununua chakula ama mahitaji mengine. Ikiwa hutoweza kupata bidhaa zingine, unastahili kufanya kile unachoweza kuzuia kukaribiana na wengine pale unapoondoka nyumbani.

Nina nani anayestahili kujitenga?

Yeyote atakayeonesha dalili za coronavirus - joto la juu ya nyuzi 37.8, kukohoa mfululizo au kuwa na matatizo ya kupumua na kila mmoja anayeishi kwenye nyumba hiyo anastahili kupimwa.
  • Ikiwa unaishi peke yako unastahili kusalia nyumbani kwa siku saba kuanzia siku ambayo umeanza kuonesha dalili
  • Ikiwa wewe au mtu unaeishi naye ameonesha dalili, nyumba nzima inastahili kutengwa kwa siku 14 kufuatilia dalili za Covid-19
  • Ikiwa mwengine ataumwa kipindi hiki, wataanza kujitenga kwa siku saba kuanzia siku hiyo. Kwa mfano, inaweza kuanzia siku ya tatu hadi ya 10 - wakati ambapo kujitenga kwa mtu huyo kutakuwa kunamalizika. Lakini pia siku hizo hazitaanza tena iwapo mwanafamilia mwengine atakuwa mgonjwa
  • Lakini yeyote ambaye atakuwa mgonjwa siku ya 13, atahitajika kuanza upya kujitenga kwa siku 7 kuanzia siku hiyo (ikimaanisha kwamba kwa siku 20 atakuwa nyumbani amejitenga.
Presentational white space
Mtu mwenye dalili anastahili kuishi katika chumba kinachoingiza hewa safi kupitia dirishani ambalo linaweza kufunguliwa na kutengwa na wengine nyumbani.
Pia watu wanashauriwa wasipige simu kwa wizara ya afya kusema dalili zao labda tu ikiwa wana wasiwasi.

Ni nani ambaye hastahili kutoka nje?

Karibia watu milioni 1.5 wenye hali mbaya zaidi za kiafya wanafuatiliwa na wizara ya afya na kuombwa wasitoke kabisa nje kwa karibia wiki 12.
Walio katika hatari zaidi ni:
  • Baadhi ya wa wagonjwa wa saratani
  • Wagonjwa waliopandikizwa viungo
  • Watu wenye maradhi megine ya kurithi
  • Watu wenye matatizo ya kupumua kama vile uvimbe wa fibrosisi na ugonjwa wa mapafu ambao umedumu kwa muda mrefu
  • Watu wanaopokea matibabu mengine ambayo yanadhoofisha mfumo wa kinga
  • Wanawake wajawazito wenye ugonjwa wa moyo
Serikali imesema kwamba itashirikiana na mamlaka za eneo, maduka makubwa ya kufanyia manunuzi na vikosi vya usalama kuhakikisha kwamba upatikanaji wa vyakula muhimu na dawa unaendelea.
Wengine katika nyumba hiyo hiyo wanaweza kutoka kwasababu ya kazi zao almuradi wazingatie sheria ya kutokaribiana.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?