Virusi vya corona: Tanzania imethibitisha wagonjwa wapya 196
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Wagonjwa wa virusi vya Corona nchini Tanzania wafikia 480
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza ongezeko la wagonjwa 196 wa virusi vya corona nchini humo.
Idadi hiyo sasa ndio kubwa zaidi kushinda taifa lolote lile la Jumuiya ya Afrika mashariki.
Kati ya wagonjwa hao 174 wanatoka Tanzania Bara huku 22 wakitoka kisiwani Zanzibar (ambao tayari taarifa zao zilishatolewa na waziri wa Afya wa visiwa hivyo siku ya Jumanne).
Akizungumza na vyombo vya habari bwana Majaliwa pia ametangaza idadi ya vifo kufikia 16 ikiwa ni ongezeko la watu 6 zaidi.
Vilevile amekuwa na habari njema kwa Watanzania akisema kwamba idadi ya waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi 167.
Tanzania kwa sasa inaongoza Afrika Mashariki kwa idadi ya wagonjwa ikifuatiwa na Kenya yenye wagonjwa 374, Rwanda 207, Uganda 79, Sudani Kusini 34 na Burundi 15.
Mji wa kibiashara wa Dar es salaam umetajwa kuongoza kwa idadi ya maambukizi nchini humo.
Licha ya mji huo kuwa kitovu cha maambukizi, Magufuli amesema jiji hilo la watu milioni sita ndio moyo wa mapato ya Tanzania.
"Wapo wengine wanatoa mawazo ya kuifunga Dar es Salaam, hili haliwezekani. Dar es salam ndio centre (sehemu) pekee ambapo collection (makusanyo) ya revenue (mapato) inapatikana kwa nchi yetu...Zaidi ya asilimia 80 ya mapato yanakusanywa Dar es Salaam," alisema Magufuli alipokutana na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo.
Pia alisisitiza kuwa kutokana na wingi wa wakaazi wake, ilikuwa ni jambo la kutegemewa kitakwimu kwa jiji hilo kuwa na wagonjwa wengi zaidi.
WHO yaikosoa Tanzania
Hatua hiyo inajiri baada ya shirika la Afya Duniani WHO kuikosoa Tanzania kwa kuchelewa kuchukua hatua za mapema kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.
Mkuu wa WHO wa bara la Afrika Bi Matshidiso Moeti alisema tarehe 24 Aprili kuwa kumekuwa na hofu juu ya kukua kwa kasi ya maambukizi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
"Kwa hakika tumeona kuwa watu kuacha kutangamana, pamoja na kupiga marufuku kwa mikusanyiko ya watu wengi kumechukua muda mrefu kufanyika na tunaamini kuwa hayo yanaweza kuwa ni moja ya mambo yaliyosababisha ongezeko la kasi la wagonjwa wa corona," alisema Dkt Moeti katika mkutano na wanahabari.
Hatuazilizochukuliwa kudhibiti maambukizi ni zipi?
Shule zote na vyuo vya elimu vimefungwa mpaka itakapotangazwa ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya corona nchini humo.
Pamoja na kuzuia mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa.
Magari ya usafiri wa umma hatayakiwi kujaza abiria, na wote lazima wawe wameketi vitini.
Ndege za abiria zimezuiwa kutua nchini humo.
Kuanzia Jumatatu ya Aprili 20 ni lazima kwa wakaazi wote wa Dar es Salaam kuvaa barakoa wanapokuwa maeneo ya umma.
Biashara zote za chakula jijini Dar es Salaam zinatakiwa kufunga bidhaa zao na kutoruhusu watu kula kwenye migahawa.
Ramani ya Coronavirus: Kasi ya kusambaa kwa virusi 22 Aprili 2020
Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.
Serikali ya Uganda imeaandaa maonyesho ya picha kuhusu raisi wa zamani Field Marshal Idi Amin Dada ambaye anadhaniwa kuwa ni mmoja wa madikteta hatari duniani. Hata ivyo maonyesho haya yanalenga kuonesha taswira tofauti na kuangazia mazuri aliyoyafanya. Je ni nini mtazamo wako kuusu hatua hii iliyochukuliwa na Serikali ya Uganda? Toa maoni yako Kuhusu hilii
Wapenzi kutoka Ufaransa wamekamatwa na kilo 40 za mchanga wa Sardinian katika gari lao na wanaweza kukabiliana na kifungo cha miaka 6 jela. Walisema kuwa walitaka kuondoka na mchanga nyumbani kwao na hawakujua kama wamefanya makosa. Ni kosa la jinai kwa mtu kuhamisha mchanga kutoka katika kisiwa cha Sardinia, kwa sababu mchanga unatambulika kama mali ya umma. Kwa miaka mingi, wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakilalamikia wizi wa mali asili ikiwa ni pamoja na mchanga. Wapenzi hao wanaweza kuhukumiwa kati ya mwaka mmoja jela mpaka miaka sita kwa kosa la wizi wa mali ya umma. Chini ya sheria ya mwaka 2017, biashara ya mchanga na mapambo ya bahari ni kunyume cha sheria, na faini ya yuro 3000. Polisi walikuta mchanga umewekwa kwenye chupa 14 ambazo zilitoka katika ufukwe wa Chia , kusini mwa Sardinia katika buti ya gari la wapenzi hao. Mwaka 1994, ufukwe uliopo kisiwa cha Budeli kaskazini mashariki mwa Sardinia uliwekewa zuio kwa ajili ya siku siku za mbeleni. Mamlaka ina hofu ya tani kadhaa z...
WANACHAMA wa Yanga wamemuangukia mwenyekiti wao aliyejiuzulu Yusuf Manji baada ya kukataa ombi la kuachia ngazi la kiongozi huyo. Wanachama wa klabu hiyo kutoka matawi 65 ya mkoa wa Dar es Salaam walikutana jana na kumtaka makamu mwenyekiti wao, Clement Sanga kuhitisha haraka kmkutano wa dharura. Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, ambapo kwa pamoja waliazimia kukataa ombi la kujiuzulu kwa Manji. “Wanachama hawataki Manji akae pembeni, wanataka mkutano wa dharura uitishwe siku 14 toka leo kwa mujibu wa katiba, kamati ya utendaji inakaa leo ( Jana) mchana itapitia maombi ya wanachama na kutoa maamuzi.” alisema Mkwasa. Naye Makamu Mwenyekiti wa matawi Bakili Makele alisema kuwa baada ya kutafakari barua ya Manji, ambayo inaeleza moja ya sababu ya kujiuzulu ni kutokana na afya yake, lakini wao wanasema bado wanamuhitaji. Naye Mwenyekiti wa Keko Ukombozi Joseph Kalindwa akizungumzia hilo alisema “ Manji alitukuta kipindi kigumu mno tukiwa tu...
Maoni
Chapisha Maoni