Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 01.10.2019: Martinez, Coman, Smalling, Brewster, Darmian, Kral
Wachezaji wa Barcelona walikuwa tayari ku saini mkataba na mshambuliaji wa PSG Neiymar ,27, msimu huu hali ya kwamba walikuwa tayari kuona mishahara yao ikipunguzwa kuhakikisha uhamisho huo unafanikiwa , kulingana na beki Gerrard Pique. Manchester City ni miongoni mwa klabu zinazomnyatia mshambuliaji wa Steaua Bucharest raia wa Romania mwenye umri wa miaka 21 Florinel Coman. Manchester United ina hamu ya mshambuliaji wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 21 raia wa Argentina Lautaro Martinez - Mshambuliaji huyo atagharimu Yuro milioni 111. Roma inataka kukamilisha uhamisho wa kudumu wa beki wa kati wa Uingereza Chris Smalling kwa dau la £18m. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka Man United yuko katika mkopo wa muda mrefu katika klabu hiyo ya serie A. Liverpool inafikiria uwezekano wa kuchezesha timu mbili katika mashindano mawili tofauti yatakayofanyika siku moja , katika robo fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Aston Villa huku timu hiyo pia ikishiriki ka...