Wakazi wa Dar es Salaam wazua gumzo mtandaoni vumbi la Makongo Juu nchini Tanzania

Mjadala mkali umeibuka katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania juu ya wakaazi wa mtaa mmoja jijini Dar es salaam kuhusu vumbi ambalo wakazi hao wanadaiwa kuingia nalo mjini.

Picha mbalimbali, maneno, kejeli na mizaha wikii hii vimetawala kwenye mitandao ya kijamii kama vile Twitter na Whatsapp zikionyesha namna wakaazi wa mtaa huo wanavyoonekana wakiwa na vumbi.

Ukiwa Dar waweza jua daladala ni ya njia ipi kwa kuangalia tu abiria wanaoshuka au kupanda.

Ukiona daladala abiria wengi wamevaa madela na baraghashia nyingi na wanaongea sana hiyo daladala ni ya kuelekea Temeke.Ukiona daladala wengi wanaopanda ni weupe weupe na wana meno ya rangirangi kama gold ni daladala ya kwenda Kimara & maeneo Mbezi mwisho .... Ila ukiona daladala .. wanaoshuka wamechafuka VUMBI kila sehemu usipate taabu... hizo ni daladala za MAKONGO JUU"... ni miongoni mwa ujumbe ambao umekuwa ukisambazwa katika mtandao wa Whatsapp Tanzania

Wakaazi wa eneo hilo wanadai kushangazwa kwa kufanywa wao ndio mada ya kujadiliwa na kudhani kwamba tatizo lao sasa linaweza kuonekana .

"Hii inaonyesha wazi kuwa watu wamechoka na kukerwa na inawezekana kuwa hata sio wakaazi wa Makongo juu ndio wanaandika, hao wanaotutania labda wanaweza kuwa wanatusaidia kwa namna moja au nyingine hivyo huwa tunabaki kucheka tu" mkaazi mmoja wa kitongoji hicho ameeleza.

Huku mwingine akilalamikia vikao na uvumilivu ambao wamekuwa nao kwa muda mwingi bila mafanikio huku wakijiuliza maswali mengi bila majibu.

Je, uchaguzi ujao tutamchagua mbunge huyu huyu? matatizo ni yaleyale tulipokuwa chama tawala na hata sasa mbunge wetu akiwa upinzani.

Tumekaa vikao vingi , watu wameitishwa vikao vingi, mimi pia niliacha shughuli zangu na kuhudhuria vikao hivyo.

Wale walioko barabarani tayari kuna wengine wameshavunja kuta zao kuachia barabara lakini hakuna matumaini yoyote. Kuna matajiri wengi katika nyumba za barabarani lakini hawataki kusogea au hawasogezwi.

Kwa sasa tunasubiri miujiza tu, wengi tumekata tamaa', ameeleza mkaazi wa Makongo.

'Tunafika mjini tumechafuka , unakutana wanavaa kiziba pua na kuna siku nilikutana na msichana mrembo amejifunga kanga nikashangaa ila tulivyofika kwenye lami akatoa khanga akaweka kwenye mkoba wake, hata ilinibidi niulize baada ya kutabasamu", ameongeza.

Tunaokaa pembezoni mwa barabara ni changamoto , kwenye upande wa usafi na tunaugua mafua kila siku.

Magari yetu yanaharibika sana na ukiwa na mgonjwa ni kazi, mpaka ufike kwenye lami ni changamoto na wajawazito nao wanapata shida sana.

Ni ngumu kuita au kuleta gari za kukodi huku(uber) wengi wanakataa na usafiri wa umma ni shida, kuna bajaji zaidi", Mama Brian ambaye ni mkazi wa eneo hilo alieleza.

Lakini pamoja na changamoto zote hizo, kwa nini bado watu wamechagua kuishi huko?

"Ni eneo tulivu sana, usalama upo na gharama ya nyumba sio mbaya na uzuri ni karibu na mjini, kikwazo kikubwa ni kufika mjini".

Tangazo kutoka kwa mkuu wa mkoa lilitolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam tangu mwaka unaanza, kuwa barabara ya Makongo inaenda kurekebishwa lakini mpaka sasa hakuna matumaini yoyote."




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?