Facebook kuhakiki maudhui yanayochapishwa kwa lugha za kiafrika kupambana na taarifa za urongo

Mtandao wa kijamii wa Facebook, kwa ushirikiano na shirika la kuhakiki taarifa la Africa Check, umeanza mpango wa kufuatilia taarifa bandia zinazochapishwa katika mtandao huo kwa kutumia lugha za kiasili za kiafrika.

Mpango huo uliozinduliwa mwaka jana katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika, sasa utajumuisha uhakiki wa lugha za Yoruba, Igbo, Swahili, Wolof, Afrikaans, Zulu, Setswana na Sotho.

Taarifa zitakazosadikiwa kuwa ghushi zitadhibitiwa hali ambayo itahakikisha haziwafikii watumiaji wengu wa mtandao huo ili zisisambazwe kwa urahisi.

Facebook inasema kuwa inategemea mrejesho kutoka kwa watumiaji wake kudhibiti taarifa bandia inapochambua uhalisia wa taarifa husika.

Mtandao huo wa kijamii wa umekuwa ukilamiwa vikali wa kusambaza taarika ghushi na kauli za uchochezi na chuki.
Facebook imekuwa ikilaumiwa kutodhibiti mitandao yao, sasa wajipanga kuchukua hatua

Barani Afrika pekee zaidi ya watu milioni 130 wanatumia mtandao wa Facebook.

Hivi karibuni Facebook iliunda mfumo mpya unaowalenga watu wanaoweka matangazo ya uongo kwenye mtandao huo.

Mfumo huo umekuja baada ya Martin Lewis, mwanzilishi wa tovuti ya Money Saving Expert, kushtakiwa baada ya jina na picha yake kutumika kwenye matangazo bandia kwenye ukurasa wa Facebook.

Facebook iliamua kuchangia kiasi cha pauni milioni 3 kwa ajili ya kutengeneza programu ya kupambana na wadanganyifu nchini Uingereza.

Mtandao huo pia ulichapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizochukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019.

Katika kipindi hicho cha miezi sita, Facebook ilifunga zaidi ya akaunti bilioni tatu feki - idadi ambayo inasema ni kubwa zaidi kuwahi kufungwa.

Zaidi ya ujumbe milioni saba za"chuki" pia zilitolewa katika mtandao huo wa kijami.

Kwa mara ya kwanza, Facebook pia iliripoti kuwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao ujumbe wao ulifutwa wamekata rufaa na kuongeza kuwa zingine zilirudishwa baada ya uchunguzi wa kina.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?