Tetesi za soka jumapili barani Ulaya:
Mshambuliaji wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, amekataa uhamisho wa kuelekea Roma, licha ya klabu hiyo ya Old Traford kukubali kulipa kitita kikubwa cha mshahara wake wa £560k kwa wiki.
Hata hivyo Sanchez huenda akaelekea katika ligi ya serie A baada ya Man United kumruhusu kufanya mazungumzo na Inter Milan, ambapo huenda akakubali kupunguza mshahara wake.
Maoni
Chapisha Maoni