Mbwana Samatta afunga hat-trick Ubelgiji na kuisadia KRC Genk kupata ushindi mkubwa

Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anayeichezea klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji siku ya Jumamosi aligonga vichwa vya habari baada ya kuisaidia timu yake kufunga hat-trick katika mechi ya ligi ya Ubelgiji dhidi ya klabu ya Waasland-Beveren.

Samatta alifiunga magoli hayo katika mechi ilioipatia timu yake ushindi mkubwa ugenini.

Mshambuliaji huyo alifunga goli lake la kwanza katika dakika ya 52 baada ya mchezaji mwenza Paintisil kuiweka kifua mbele KRC Genk kunako dakika ya 21.

Baadaye mshambuliaji huyo alifongeza goli la pili na la tatu kwa jumla katika dakika ya 66.

katika ukurasa wake wa instagram Samatta aliandika: Ni Furaha kupanta pinti tatu muhimu leo nje ya nyumbani. Timu ilkicheza vizuri. Na tunawashukuru mashabiki waliosafiri kutupa sapoti.Pia nina furaha kufunga hat-trick yangu ya kwanza msimu huu na nina imani nyingi zitakuja.

Ruka ujumbe wa Instagram wa samagoal77

Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa samagoal77

Lakini hakusita hapo kwani muda wa dakika za lala salama kiungo huyo matata alifunga goli lake la tatu na kuipatia timu yake ushindi wa magoli 4-0.

Katika akaunti yake ya Facebook mshambuliaji huyo mahiri aliandika: Hat-Trick yangu ya kwanza nikiwa na KRC Genk tena ugenini msimu mpya nauwashaaa, huku akionekana kuirejelea kauli yake ya 'haina kufeli'.
Miezi iliopita mchezaji huyo alizivutia klabu za Uingereza kama vile Aston Villa Watford, Leicester na Burnley baada ya kuonyesha hamu yake ya kutaka kujiunga na klabu za ligi ya Uingereza.

Klabu ya Brighton imekuwa ikimfuatilia Samatta kwa muda mrefu na kocha wa timu hiyo kwa msimu uliopita Chris Hughton alikuwa akivutiwa sana na mchezaji huyo.

Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe Januari 2016 ambapo alitia saini mkataba wa kumuweka katika klabu hiyo hadi msimu wa 2019/20.

Msimu uliopita, 2018/19 bila ya shaka ulikuwa bora kabisa kwake toka alipojiunga na klabu hiyo.

Alifunga magoli 23 ya ligi na magoli 9 kwenye michuano ya ligi ya Europa. Pia amepata tuzo ya Ebony ambayo hutuzwa mchezaji bora mwenye asili ya Afrika nchini Ubelgiji.

Pia ametoa mchango mkubwa kwa klabu hiyo kuchukua ubingwa wa ligi baada ya kuukosa kwa miaka minane.

Samatta alianza Maisha yake ya soka akiwa kinda na klabu ya Mbagala Market kisha akasajiliwa na Simba zote za Dar es Salaam Tanzania. Mazembe walimsajili 2011 akitokea Simba.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Watalii wa Ufaransa kukabiliana na hukumu ya wizi wa mchanga