Rais wa Tanzania John Magufuli ndiye mwenyekiti mpya wa SADC

Rais wa Tanzania, John Magufuli ndiye mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC.

Bw. Magufuli ambaye amekabidhiwa uwenyekiti huo na Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob ataongoza Jumuiya hiyo kwa mwaka mmoja.

Akipokea uwenyekiti huo Rais Magufuli amesema:''Tunaahidi kushirikiana na nchi zote Wanachama wa SADC kuhakikisha kupitia mkutao huu ndoto na mawazo ya Baba wetu wa Taifa pamoja na viongozi wengine waanzilishi wa Jumuiya hii yanaendelea kutekelezwa kwa vitendo''

Tayari mwenyekiti huo mpya ameomba rasmi Jamii ya Kimataifa kuiondolea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumu akiongezea kuwa vikwazo hivyo vimelemaza uchumi wa taifa hilo

Kwa mujibu wa Bw. Magufuli vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe vinaathiri pia ushirikiano wake katika Jumuiya ya Sadc na kuomba nchi hiyo ipewe nafasi ya pili kwa sababu ina utawala mpya.

Rais wa nchi hiyo Emerson Mnangagwa pia yuko nchini Tanzania kuhudhuria mkutano huo wa siku mbili.

Zimbabwe iliwekewa vikwazo hivyo na mataifa ya Magharibi miongo miwili iliyopita kufuatia hatua ya rais Robert Mugabe kuchukua kwa lazima ardhi ya walowezi wa kizungu.

Mwenyekiti huyo mpya ameapa kuhakikisha amani na uthabiti unadumishwa katika kanda hiyo ili kukwamua uchumi wa mataifa wanachama

Pia ametoa wito kwa nchi wanachama kushirikiana kibiashara badala ya kuagiza bidhaa kutoka nje.

''Narudia tena kuwakaribisha waheshimiwa wakuu wa nchi kwenye mkutao huu wa 39 wa SADC hapa Dar Es Salaam mahali penye amani ambapo ni kitovu cha harakati za ukombozi Barani Africa'' alisema Magufuli

Kiswahili pia kimetangazwa kuwa lugha ya nne rasmi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc)

Lugha zingine rasmi katika Jumuiya ya SADC ni Kiingereza, Kifaransa na Kireno.

Hapo jana Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini walitangaza kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kirafiki baina ya mataifa hayo mawili wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC

. Magufuli na Ramaphosa pia walitoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini kuwekeza kikamilifu kwenye nchi hizo.

Tayari rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameanza kutumia lugha ya Kiswahili kwenye Twitter yake akielezea jinsi alivyopokelewa nchini Tanzania ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa 39 wa kilele wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC.

Viongozi pia wanatarajiwa kujadili masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na Usalama katikakanda ya Kusimi mwa Afrika na uchimi wake. Mkutano wa leo inaadhimisha miaka 17 kubuniwa kwa Jumuiya ya maendeleo ya matifa ya kusini mwa Afrika.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?