Nusu ya dhahabu inayonunuliwa kwa wachimbaji wadogo Chunya inatoroshwa:

Zaidi ya nusu ya dhahabu inayonunuliwa na wanunuzi wa kati maarufu kama Brokers kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo wilayani Chunya  inatoroshwa badala ya kupelekwa kuuzwa kwenye soko kuu la dhahabu lililofunguliwa na serikali wilayani humo.
Licha ya serikali kufungua soko la madini wilayani Chunya kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji na wanunuzi wa dhahabu kufanya biashara hiyo kwa njia halali na serikali kupata mapato yake, imebainika kuwa madini ya dhahabu hasa yanayonunuliwa kutoka kwa wachimbaji wadogo hayafikishwi sokoni hapo na badala yake yanatoroshwa  na kwenda kuuzwa nje ya wilaya na hata kusafirishwa nje ya nchi kinyemela.

Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilaya ya Chunya, Luitufyo Mwambungu amesema utoroshaji huo wa dhahabu una harufu ya kuambatana na vitendo vya rushwa na kuwataka wananchi kutoa taarifa za vitendo hivyo, huku Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania, TRA, wilaya ya Chunya, Osaund Mbilinyi akidai kuwa ipo changamoto ya wanunuzi na wachimbaji wa madini kutokuwa na mwitikio wa kulipa kodi.
Afisa Madini mkazi wa wilaya ya Chunya Gibson Kamihanda amewataka wale wote wanaojihusisha na utoroshaji wa dhahabu wilayani humo kuacha tabia hiyo mara moja kwa vile adhabu yake kisheria ni kali kiasi cha kuwafilisi na kuwaondoa kabisa kwenye biashara ya madini.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?