Ubaguzi dhidi ya Pogba: Wito watolewa wachezaji kususia mitandao ya kijamii

Mkufunzi wa timu ya soka upande wa akina dada nchini England Phil Neville amesema kuwa wachezaji wanapaswa kususia mitandao ya kijamii ili kutuma ujumbe mzito kwamba ubaguzi wa rangi hautakubaliwa.

Matamshi ya Neville yanajiri baada ya kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba kupokea machapisho ya ubaguzi wa rangi mitandaoni kufuatai hatua yake ya kukosa penalti wakati wa mechi iliotoka sare ya 1-1 dhidi ya Wolves siku ya Jumatatu.

''Lazima tuchukue hatua mwafaka sasa kama jamii ya kandanda. Tumeona na wachezaji wangu katika mitandao ya kijamii, ligi ya Premia na mabingwa wameona'' , alisema Neville.

''Sijui kama jamii ya soka tunafaa kususia mitandao ya kijamii , kwa sababu Twitter haitachukua hatua yoyote, instagram haitafanya lolote - wanakutumia barua pepe wakisema kwamba watachunguza lakini hakuna kinachofanyika''.

Nimepoteza imani na yeyote anayeendesha idara za mitandao hii, hivyobasi tutume ujumbe mzito. Tususie mitandao ya kijamii kwa miezi sita. Tuone athari yake kwa kampuni hizo za mitandao ya kijamii''.

Siku ya Jumanne, Twitter ilitoa taarifa ikisema kuwa inashutumu kwa nguvu matusi na sasa imepiga marufuku baadhi ya akaunti kwa kukiuka sera yake ya chuki.

Iliongezea: Tunajua kinachoendelea kuhusu ubaguzi wa rangi mitandaoni dhidi ya wachezaji fulani nchini Uingereza katika siku za hivi karibuni.

Tunachunguza matamshi hayo na tutaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya akaunti yoyote inayokiuka sheria. Hili ni swala la kijamii na linahitaji jamii kuchukua hatua.

Hii ndio sababu tunaendelea mjadala na muungano wa wachezaji wa kulipwa pamoja na Kick it out na wako tayari kushirikiana kutatua matusi mitandaoni na tabia za kibaguzi katika sekta hii.

Taarifa kutoka kwa facebook ilisema: hakuna nafasi ya ubaguzi ama tabia ya matusi katika instagram na tunawekeza pakubwa katika kuimarisha vifaa na teknolojia ili kuzuia uonevu na unyanyasaji.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walianzisha kampeni ya #istandwithpogba

Watu ambao huvunja maelezo yetu watapigwa marufuku kutotumia Instagram.

Wachezaji wenza wa Pogba wamekosoa matusi hayo dhidi ya raia huyo wa Ufaransa , ambaye penalti yake ya dakika ya 68 iliokolewa na kipa wa Wolves Rui Patricio - ikiwa ni penalti ya nne iliopotezwa na mchezaji huyo akiichezea United katika ligi ya Premia tangu msimu uliopita.

Harry Maguire alitaka kampuni za mitandao ya kijamii kusitisha kujifanya kwamba zina huruma huku Marcus Rashford akisema kwamba inatosha na swala hilo linafaa kukomeshwa.

''Manchester United ni familia. Pogba ni mwanachama wa familia ,unapomshambulia munatushambulia sisi sote'', mshambuliaji huyo wa England aliongezea katika mtandao wa twitter.

United imesema kwamba inatumia kila mbinu kuwafichua wale waliomtusi Pogba.

Watu waliowasilsha maono hayo hawaungi mkono maadili na thamani ya klabu yetu na inatupa moyo kuona kwamba idadi kubwa ya mashabiki wetu wameshutumu hilo katika mitanfdao ya kijamii , ilisema taarifa ya United.

''Tutafanya kazi kubaini watu wachache waliohusika katika visa hivi na kuchukua hatua kali. Tunazitaka kampuni za mitandao ya kijamii kuchukua hatua dhidi ya kesi kama hizi''.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?