Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2020

Virusi vya corona: Tanzania imethibitisha wagonjwa wapya 196

Picha
Wagonjwa wa virusi vya Corona nchini Tanzania wafikia 480 Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza ongezeko la wagonjwa 196 wa virusi vya corona nchini humo. Idadi hiyo sasa ndio kubwa zaidi kushinda taifa lolote lile la Jumuiya ya Afrika mashariki. Kati ya wagonjwa hao 174 wanatoka Tanzania Bara huku 22 wakitoka kisiwani Zanzibar (ambao tayari taarifa zao zilishatolewa na waziri wa Afya wa visiwa hivyo siku ya Jumanne). Akizungumza na vyombo vya habari bwana Majaliwa pia ametangaza idadi ya vifo kufikia 16 ikiwa ni ongezeko la watu 6 zaidi. Vilevile amekuwa na habari njema kwa Watanzania akisema kwamba idadi ya waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi 167. Tanzania kwa sasa inaongoza Afrika Mashariki kwa idadi ya wagonjwa ikifuatiwa na Kenya yenye wagonjwa 374, Rwanda 207, Uganda 79, Sudani Kusini 34 na Burundi 15. Mji wa kibiashara wa Dar es salaam umetajwa kuongoza kwa idadi ya maambukizi nchini humo. Licha ya mji huo kuwa kitovu cha maambukizi, Magufuli ames