Eric Kabendera: Mwandishi wa Tanzania kuendelea kuzuiliwa baada ya mahakama kuahirisha kesi dhidi yake
Mwandishi wa habari za uchunguzi , Erick Kabendera ataendelea kuzuiliwa jela baada ya Kesi ya uhujumu Uchumi inayomkabili ikuahirishwa hadi Septemba 12 mwaka huu. Hii ni baada ya upande wa Serikali kudai kuwa upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika.Wakili wake Jebra Kambole ameiambia Mahakama ya hakimu Mkaazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa waleta mashtaka wanapaswa kuhimizwa wakamilishe upelelezi kwa Wakati na kuiomba Mahakama isisitize juu ya Hilo Wakili Kambole pia amesema kuwa afya ya Kabendera ianendelea kuzorota baada ya kupata tatizo la upumuaji inapofika usiku tangu Agosti 21 hali iliyomfanya kushindwa kutembea kwa siku mbili. Aidha ameiomba Mahakama hiyo iliamuru Jeshi la Magereza kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili mtuhumiwa ili aweze kupatiwa vipimo. ''Kwa kuwa mteja wetu hajapata huduma ya matibabu tunaomba Mahakama ielekeze maafisa wa magereza kumpeleka katika hospitali yoyote ya serikali akapimwe '' alisema wakili huyo. Hata hivyo Wakili wa Serikali, Simon...